Na matukio daima App,
Watu watatu wamehukumiwa adhabu ya kifo, akiwamo mke aliyemkodi kaka yake na mtu mwingine kisha kuwalipa Sh100,000 ili wamuue mumewe kwa madai alikuwa akifuja mali ya familia kwa kuuza vyakula na kwenda kunywa pombe.
Mshtakiwa huyo wa kwanza, Rehema Maksoni alimkodi kaka yake, Ajuaye Maksoni na Shadrack Paschal ambao walimchoma mumewe Lameck Makupi na kitu chenye ncha kali tumboni kilichosababisha utumbo mkubwa kutoka.
Ilidaiwa mahakamani hapo Rehema alipokamatwa na kuhojiwa alikiri kupanga mauaji ya mumewe akidai alikuwa akifuja mali ya familia kwa kuuza vyakula na kutumia fedha hizo kunywa pombe hivyo alimchoka.
Hukumu hiyo imetolewa jana Jumatatu Septemba 23, 2024 na Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma mbele ya Jaji John Nkwabi, aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo.
0 Comments