Header Ads Widget

MCHENGERWA: VIJIJI 12,33,MITAA 4,269 NA VITONGOJI 64,274 NDIVYO VITAKAVYOSHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.

NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA 

 Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala la mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa ametoa amri ya mgawanyo wa maeneo ya utawala katika serikali za mitaa  ambapo  jumla ya vijiji 12333, Mitaa 4269 na vitongoji 64274 ndivyo vitakavyo shiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.



Mchengerwa ametoa amri hiyo leo Septemba 16 wakati akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha ambapo alisema kuwa amri hiyo inajumuisha maeneo yaliyokuwa yamefutwa awali kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 673 na 674, mojawapo ikiwa ni Tarafa ya Ngorongoro



 Alieleza kuwa Lengo la hatua hiyo ni kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanapata uwakilishi mzuri wa kiutawala, pamoja na huduma za kijamii na kiuchumi zinazowiana na mahitaji ya wananchi ambapo Notisi hizo ndizo ambazo zimeainisha mitaa, vitongoji, na vijiji vitakavyoshiriki katika uchaguzi huo



"Amri ya Mgawanyo wa Maeneo ya Utawala katika Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) (Tangazo la Serikali Na. 796 la mwaka 2024) imetolewa kwa mujibu wa kifungu cha 30 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura ya 287.

Notisi ya Mgawanyo wa Maeneo ya Utawala katika Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) (Tangazo la Serikali Na. 797 la mwaka 2024) imetolewa kwa mujibu wa vifungu vya 16(1) na 18(1) vya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288.

Matangazo haya yanajumuisha maeneo yaliyokuwa yamefutwa awali kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 673 na 674, ambayo yalihusisha pia Tarafa ya Ngorongoro," Allitangaza Mchengrwa.


Aidha aliwasisitiza wananchi  kuona umuhimu wa kujitokeza kwa wingi kwa wale wote wenye sifa ili kushiriki kikamilifu katika kuunda serikali ya wananchi kidemokrasia ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanajiorodhesha katika Orodha ya Wapiga Kura ifikapo Oktoba 11 hadi 20, ambayo itatumika siku ya uchaguzi October 27.


"Pia nawahimiza wale wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika Serikali za Mitaa kuchukua hatua za mapema za kujiandaa na kushiriki kikamilifu kwani mchakato huu ni fursa kwa wananchi kushiriki moja kwa moja katika kuamua mustakabali wa maendeleo ya maeneo yao lakini inahitjika kupata  uongozi imara katika ngazi ya mitaa, vitongoji na vijiji  ili kuendeleza juhudi za Serikali za kujileta maendeleo endelevu," Alieleza.



Kwa upande wake mkuu wamkoa wa Arusha Paul Makonda alisema kuwa  kama mkoa watahakikisha wanatendea kazi amri hiyo ili  wananchi wa mkoa wa Arusha na watanzania kwa ujumla wapate nafasi ya kuwachagua viongozi wanaowataka  kwaajili ya maendeleo ya nchi.



Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Mmarekani Bayo alisema kuwa wamelipokea kwa furaha tangazo hilo kwani wananchi wataweza kupata haki ya kuchagua kiongozi wanayemtaka ambapo pia wataendelea kuhamasisha wananchi wa wilaya hiyo kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wakazi la mpiga kura.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI