NA NAMNYAK KIVUYO, LONGIDO
Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa Mohamed Mchengerwa amewataka wakuu wa mikoa ya mipakani kuimarisha ulinzi na usalama ili kudhibiti matukio mbalimbali yanayoweza kuleta madhara ikiwa ni pamoja na
kudhibiti Homa ya Nyani (Mpox) kwa kupima ugonjwa huo kila mgeni anayengia nchini.
Mchengerwa alitoa agizo hilo leo Septemba 18,2024 wilayani Longido, mkoani Arusha katika ziara yake ambapo alisema kuwa ni vema ulinzi ukahimaroshwa zaidi maeneo yote ya mipaka ili kuhakikikisha hakuna matukio yanayoweza kutokea na kuharibu taswira ya nchi.
Alisema kunabaadhi ya watu wanahujumu nchi kwa kuingiza magendo hususan maeneo ya mipakani hivyo alipongeza Mkuu wa Mkoa wa Mkoa ,Paul Makonda kwa kutoa mafuta lita zaidi ya 25000 kwaajili ya kuimarisha ulinzi ikiwemo kutoa mafuta kwa vyombo vya ulinzi na usalama na huo ndio ubunifu unaotakiwa kwaajili ya kuhakikikisha ulinzi na usalama unaimarishwa.
"Hakikisheni mipaka yetu hass mpaka wa Kituo cha Forodha cha Pamoja (OSBP) Cha Namanga kinakuwa salama lakini pia tambueni kuwa tunachangamoto ya ugonjwa wa homa ya nyani (Mpox)ambao upo nchi jirani hivyo imarisheni usalama maeneo ya mipakani kwani ugonjwa huu haupo mbali upo jirani ya nchi zetu hivyo msingi wa kuimarisha mipaka yetu utatusaidia kudhibiti ugonjwa huu kwakushirkiana na Wizara ya Afya"
Aliagiza kukaguliwa kwa wageni wanaoingia nchini kwenye maeneo ya mipakani ili kudhibiti ugonjwa wa Mpox nabtaratibu nyingine zs kiafya zichukuliwe ikiwemo kudhibiti magendo yanayoingia mipakani na anayetoa pia tumjue.
"Lazima tutambue wageni wanaoingia na kutoka ikiwemo vitu vinavyoingia na kutoka huku jambo la mashine ya ukaguzi (scanner) analichukua na kuongea na Waziri wa Fedha,Mwigulu Nchemba ili kurekebisha tatizo hili haiwezekani nchi ya Kenya wanascaner lakini nchi ya Tanzania ikiwa haina mashine hiyo na hujui kinaingia "
Aidha kuhusu changamoto ya scaner alisema ataongea na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba kwaajili ya kuhakikikisha scanner hiyo inafika mpakani Namanga hapo mara moja
Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda alisema Mkoa huo umejipanga katika kuhakikikisha unatatua chagamoto ya maji kwa wananchi kutengewa maeneo ya mifugo kunywa maji na kwakuanzia Wilaya ya Ngorongoro umeanza utekelezaji huo kwa visima 17 kutengewa maeneo ya mifugo kunywa maji na kuondoa changamoto kati ya wafugaji na wakulima.
"Pia mkoa kwa sasa upo katika hatua ya tatu ya kulima kilimo cha nyasi ili kuondoa changamoto ya mifugo kukosa chakula na kutembea umbali mrefu kupata malisho kwani mifugo lengo letu ni tuondokane na migogoro baina ya wafugaji na wakulima ikiwemo upatikanaji wa maji kwa mifugo yao kwani kwa Mkoa huu mifugo ni siasa hivyo tumekuwa na awamu ya tatu ya ulimaji wa kilimo wa nyasi," Alisema
Naye mkuu Wilaya wa Longido Salum Kali alisema wilaya hiyo iliyopo mpakani mwa Tanzania na Kenya umejipanga kukabiliana na ugonjwa huo sanjari na uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwemo kuhakikisha inatatua changamoto ya wananchi kukata mabomba ya maji ambapo kwa zaidi ya siku tatu zilizopita wananchi walikata mabomba hayo ili kunywesha mifugo yao.
0 Comments