Header Ads Widget

MABORESHO MAKUBWA HOSPITALI YA MJI KASÙLU

Kiongozi wa mbio za mwenge Godfrey Mnzava (kushoto) akiweka jiwe la msingi la ukarabati wa majengo ya hospitali ya mji Kasulu

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

UKARABATI mkubwa unaofanywa kwenye hospitali ya wilaya ya halmashauri  ya mji wa Kasulu mkoani Kigoma unaelezwa kuwa  utaimarisha utoaji huduma katika halmashauri hiyo na kupunguza rufaa ya wagonjwa kwenda hospitali ya rufaa ya mkoa kigoma Maweni.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya mji wa Kasulu,  Jaffari Makombe akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la mradi huo na kusema kuwa utekelezaji wa mradi huo unatokana na fedha kiasi cha shilingi milioni 900 zilizotolewa na serikali.

 

Makombe alisema kuwa jumla ya majengo 19 yanahusika kwenye ukarabati huo ambapo kwa sasa tayari majengo Matano yamekamilika na yameanza kutoa huduma, majengo yatakamilika mwishoni mwa mwezi huu na majengo manane kuanza ukarabati mwezi Oktoba.

 

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi la mradi huo Mbunge wa jimbe la Kasulu Mjini,Prof. Joyce Ndalichako alisema kuwa Pamoja na ukarabati huo Mkubwa wa hospitali ya halmashauri pia serikali imeweza kujenga vituo viwili vipya vya afya na zahanati 10 jambo linalochangia kusogeza huduma za matibabu karibu na wananchi.

 

Profesa Ndalichako alisema kuwa uboreshaji huo wa miundo mbinu ya afya katika jimbo hilo kunakofanywa na serikali kunaimarisha mpango wa serikali wa utoaja wa huduma bora za afya.

 

Kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi huo kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2024, Godfrey Mnzava alitoa maelekezo kwa wasimamizi na watumishi wa idara ya afya katika halmashauri ya mji wa kasulu kuzingatia weledi na juhudi katika utoaji huduma ili kiasi kikubwa cha fedha kinachotolewa na serikali katika uboreshaji wa miundo mbinu ya kutolea huduma viende sambamba na utoaji huduma bora kwa weledi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI