Mbunge wa jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma Felix Kavejuru (kulia) akitoa wosia kwa mtoto wake German Felix wakati wa sherehe ya kumuaga mtoto huyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii mjini Kigoma
Na Fadhili Abdallah, Kigoma
WITO umetolewa kwa wanandoa wapya wanaooana sasa kushika mafundisho ya dini zao katika utii na heshima ili kuzifanya ndoa zao zidumu.
Mbunge wa jimbo la Buhigwe Felix Kavejuru alisema hayo akitoa wosia kwenye harusi ya kumuaga binti yake,Germana Felix iliyofanyika kwenye kanisa la Anglikana mjini Kigoma.
Kavejuru alisema kuwa watoto wanaoelelewa kwenye misingi ya mafundisho ya dini wamekuwa wakitafakari inapotokea migogoro ya ndoa na kuwashirikisha viongozi wa madhehebu yao ambao wamekuwa msaada mkubwa katika kuokoa ndoa nyingi zisivunjike.
Katika wosia wake kwa mtoto wake huku akinukuu kitabu kitakatifu cha Biblia Kavejuru amemwambia mtoto huyo kuwa anapaswa kufuata mafundisho ya ndoa aliyopata kutoka kwa walimu wa dini wa kanisa katoliki (Makatekista) ambao walimpa mafundisho ya ndoa kabla hajafunga ndoa.
Mbunge huyo alisema kuwa takwimu mbalimbali zinaonyesha kuwepo kwa changamoto kubwa kwa wanandoa hasa wanandoa vijana ambapo alisema kuwa anaamini misingi mizuri ya dini kwa wanandoa inaweza kuwa suluhu kubwa ya kuzuia ndoa nyingi kuvunjika.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Kirumbe Ng’enda alimpongeza Mbunge Kavejuru kwa hatua ya kufanikisha ndoa ya binti huyo huku akimtakia Maisha mema, marefu na yenye furaha kwenye ndoa yake.
Mwisho.
0 Comments