Header Ads Widget

MACHIFU WAIOMBA SERIKALI KUWAREJESHEA MISITU YA ASILI WAITUNZE ILI KUTUNZA MAZINGIRA

 

Chifu wa mkoa wa Mbeya Rocket Mwashinga akisalimiana na Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga wakati wa Tamasha hilo

Baadhi ya mama lishe na Baba lishe walioshiriki shindano la mapishi Jijini Mbeya

Na  Matukio Daima Media, Mbeya 

KIONGOZI wa Machifu  Mkoa wa 

Mbeya Chifu ,Rocket Mwashinga ameiomba Serikali kuwarejeshea maeneo ya 

misitu ya asili wayatunze  ndani ya miaka mitano ili warejeshe uoto wa asili uliopotea kutokana na uhalibifu wa mazingira  katika maeneo  mbalimbali hapa nchini .


Chifu Mwashinga amesema hayo Agosti 31,2024 wakati wa hitimisho la mashindano ya mapishi ya chakula kwa Mama Lishe na Baba 1000 kutoka kata 36 Jijini Mbeya ambalo limeandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust chini Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini na Rais umoja wa Mabunge Duniani (IPU)mbaye pia ni Mkurugenzi Taasisi hiyo.


"Serikali ituwezeshe sisi machifu kulinda mazingira kwani tuna uwezo mkubwa sana na tukisimama imara na kurudisha uoto wa asili na  utunzaji mazingira utakuwa vizuri katika maeneo yote "amesema Chifu Mwashinga.


Amesema kuna kipindi akiwa Dodoma alizungumzia  ndani ya miaka 10 machifu wote wakishirikiana kulinda mazingira nchi  itakuwa kijani  na kuomba nishati ya gesi  waliyoleta ipungue bei ili  kuendelea kuokoa mazingira.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameipongeza Taasisi ya Tulia Trust kwa kuendelea kuleta  tija kwa Mama lishe na Baba Lishe  wa Mkoa wa Mbeya katika shughuli zao na  kuwajenga kiuchumi pamoja na jitihada za kutunza mazingira.

Kapinga amesema Tamasha hilo ni mwendelezo wa jitihada za serikali  ya awamu ya sita katika kuhamasisha.matumizi ya nishati safi ya kupikia na serikali imeandaa mkakati wa kufikia zaidi ya asilimia 80  wawe wanatumia nishati safi ya kupikia na  inaendelea na kampeni  ili kuhakikisha inawafikia watanzania wengi zaidi .

Hata hivyo Kapinga ameeleza kuwa mwaka 2023  ilianza kutoa Ruzuku ya mitungi ya gesi  ambapo  mwaka uliopita walitoa mitungi ya gesi 104,000 .

Kwa upande wake Shekhe wa msikiti wa Isanga ,Ibrahim Bombo amesema kuwa kama viongozi wa dini wataendelea kushirikiana naDkt ,Tulia katika kulinda na kutunza mazingira kwa kuhamasisha matumizi Bora ya nishati safi ya Gesi .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI