MWANDISHI WETU, - MATUKIO DAIMA APP
Matukiodaima3@gmail.com
MATAMSHI yaliotamkwa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM )BALOZI Dk Emmanuel Nchimbi katika mkutano wake na Wahariri wa Vyombo vya habari yamesaidia mno shusha joto na upepo wa taharuki ya kisiasa nchini.
Amejitahidi kadri ya uwezo wake kulileta taifa pamoja dhidi ya tisho la mgawanyiko unaopigiwa chapuo baadhi ya watanzania walioko nje ya nchi.
Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na piga nikupige ya kuturushiana maneno makali katika jamii kwa maneno yenye jazba yakikosa ukweli matiki ya kujenga umoja wa Kitaifa.
Mfululizo wa kuripotiwa watu kutekwa na kwenda kusikojulikana ,kumezidisha i wasiwasi na hofu ikiwemo tukio la kuuawa kwa Mjumbe wa sekreteriet ya CHADEMA marehemu Ali Mohamed Kibao .
Kifo cha Kibao kilikaribia kuzidisha chuki na hamaki lakini pia kuibuka kwa mabishano yaliokuwa na mitazamo hasi baada ya kutanda huzuni, mlajonzi na hofu.
Kwa watu waliomsikiza kwa umakini Dk Nchimbi, wamemsikia alioyanena Ametamka maneno mazima yatokanayo na ukweli wa historia ya nchi yetu tokea kuzaliwa kwa jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 1964
Yalikuwa ni matamshi yenye mpangilio na sentensi zenye mashiko. Hotuba yake ya saa kadhaa ,yamebeba ukweli na uhalisia wa mambo jinsi yanavyotakiwa yawe muda wote .
Amekutana waandishi wa habari katika wakati muafaka.Ameitendea haki hadhira aliokutana nayo ,na kupitia mkutano wake huo dhamira ya Dk Nchimbi imeeleweka na kila mtu aliyemsikia.
Kutokana na maelezo yake amejiandaa kabla hajitokeza kwa muda sahihi .Dk Nchimbi hakukurupuka ila yaonyeaha amesema anakwenda kusema Taifa limsikie.Kwa hakika kabla ametafakari kisha akasema .
Hakutaka kabisa kusema ili ionekane amesema, badala yake amepania kusema anayoyaamini na kuweza kuyatetea kwa nguvu ya hoja .
Amekuja mbele ya Taifa ilhali akiwa na maneno kamili ya kusema na hakika amesikika . Hivyo watanzania nao hawanabudi kumsikiza aliyoyasema na kuyazingatia.
Katibu mkuu huyo wa ccm kwa kiasi kikubwa amefanikiwa kushusha joto zito lililotandaa kwenye Taifa kufuatia matukio ya kutisha. .
Amesafisha upepo yabisi na kulirudisha taifa juu ya mstari.
Ametumia maneno mazuri na kutoa mifano hai ,misamiati adimu lakini yenye ukweli utokanao na mapitio ya historia ya Taifa letu.
Ameizungumza kwa ufupi lakini kwa undani wa historia ya usalama wa nchi yetu
.Ametaja misukosuko migumu iliolikumbana taifa lakini kwa bahati tukavuka pamoja .
Licha ya nchi yetu kupitia dhoruba kali lakini tumerudi tukiwa pamoja.Tumebaki na umoja weru kwa miaka yote sitini ya kujitawala kwetu.
Vilevile Katibu huyo mkuu ameonyesha juhudi ,bidii na kazi ngumu ya jeshi la polisi miaka kwa miaka likisimamia uliizi wa nchi na usalama wa raia na mali zao.
Ni kweli kuna baadhi ya nyakati mambo huendeshwa kisengere nyuma katika baadhi ya wakati .Mambo mengine tunajua hufanyawa na baadhi tu ya askari wazembe wasioheshimu misingi ,maadili, taratibu na nidhamu ya jeshi hilo .
Kwa sehemu kubwa askari wa aina hiyo ndiyo wanaolipaka nuksi na mikosi jeshi la polisi kwa kwenda kinyume na mafunzo, mfumo ,kanuni ,taratibu na heshima ya polisi.
Kazi za polisi si za kimzahamzaha. Kila polisi hutakiwa kufuata taratibu zilizowekwa ilkutimiza haki na wajibu wa kutumikia watu wananchi na marufuku kufanya maonevu au kubambikia watu kesi .
Kazi za polisi ni ngumu lakini pia ni nyepesi ikiwa polisi mhusila atatimiza kazi zake lwa mujibu sheria na utii wa katiba ya nchi.Polisi ndio wenye haki ya kuwalinda raia.
Polisi hutakiwa kujua na kuhakikisha usalama raia , mali zao na Taifa zima usiku na mchana tokea tulipojitawala zipo mikononi mwao
Si kwamba Dk Nchimbi ameeleza kwa hisia kali bali pia ametumia lugha ya kiungwana na kidiplomasia iliokuwa fasaha na kueleweka .Kisaikoljia na kifikra ameonyesha kukerwa na matukio yanayotajwa kutokea.
Amelikumbusha Taifa kwa kuonyesha maarifa ,ukomavu na upeo alionao kisiasa na kionngozi ikiwemo kutumia hekima na busata alizojaaliwa .
Kujitokeza kwake mbele ya Wahariri hakwenda kwa kutumia mkongojo au kutetea sera za chama chake ,ameulizwa maswali mazito na kujibu kwa uwazi na kujiamini.
Amejibu kwa mintarafu ya kujenga taifa, kuziba nyufa na kujenga ukuta.
Kwani kiongozi huyo amezumgumza ukweli mtupu akioyesha jinsi asivyoridhika kwa mambo yaliotokea .
Amekumbusha haki na wajibu kwa kila moja kua dhamana alionayo na kulinda thamani ya utu, ubinadamu wa kila mmoja .
Ametaka haki za binadamu zilimdwe na kuheshimu utawala wa sheria.
Aidha hotuba ya Dk Nchimbi pamoja na maswali alioulizwa kujibu , hayawezi kutiliwa shaka aidha na viongozi wenzake wa kisiasa, dini, mashrika hiari ya kijamii ,jumuiya za kimataifa na wanadiplomasia kwa kile alichokieleza.
Maelezo yake yana ufafanuzi aliotokana na taharuki iliokuwepo katika kichaka cha hofu , ni maneno yaliohitimisha utata wa sakata zima huku akiliachia kazi jeshi la polisi lijipange .
Wapo waliotazamia pengine wanasiasa wenzake wa vyama vingine nao wakitokeza ili kuyauga mkono matamshi hayo bila kujali itikadi za kisiasa na mitazamo ya vyama vyao.
Ikiwa tulijenga Taifa pamoja huku tukikomboa mataifa mengine, tukakabili majanga ya ukame, vimbunga ,mvua,jau, mafuriko hadi kufikia kula mahindi ya njano ,hatimaye tulivuka salama ,hivyo hakuna gumu linalotushinda jama tutaendelea kulinda misingi ya amani na umoja wa Kitaifa.
Tumepambana kwa gharama kubwa kupinga ubaguzi wa rangi kusini mwa Afrika;tulipaza sauti kukemea ukandamizaji haki, mauaji huko Mashariki ya Kati na kila pembe ya dunia .
Tutukipigania pqmoja haki za binadamu wenzetu na kusimama kwenye vyombo vya kimataita tukisema kama Taifa ,hivyo basi katu watanzania tusikubali kugawanywa na kugawanyika.
0 Comments