Header Ads Widget

MAKALA:KWANINI UTALII WA PUTO NI KIVUTIO MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA HIFADHI YA RUAHA ?

Na Matukio Daima App 

Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, mojawapo ya vivutio muhimu vya utalii nchini Tanzania na Hifadhi hii itaendelea kuwa Hifadhi ila wengi wanajiuliza kwanini utalii wa puto (hot air ballooning)ni kivutio Kikubwa maadhimisho ya Miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha?

Ifahamike kuwa Hifadhi ya Ruaha iliyoko wilaya ya Iringa  mkoa Iringa, ni hifadhi ya pili kwa ukubwa nchini, ikifunika eneo la kilomita za mraba 19,822 na kuwa na bianuai kubwa inayovutia watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Kwa taswira hiyo Pekee Hifadhi hii inajitosheleza kuwa na sifa za ubora Kuliko Hifadhi nyingine zinazofuata kwa ukubwa baada ya Ruaha .

Pamoja na uzuri huo bado ubunifu zaidi wa kuvutia watalii ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha umeendelea kufanyika bila kuathiri mazingira ya Hifadhi hii sasa inakuja Teknolojia ya utalii kwa watalii ya utalii wa Puto.



Teknolojia hii inakuja ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya kwanza kufanyika ya Miaka 60 ya Hifadhi hii ya Ruaha  yatakayofanyika kuanzia tarehe 1 hadi 7 Oktoba 2024 kutarajiwa  kutamatishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana.

Ni vizuri  kama ulikuwa hujui ama unajua basi ukajuzwa zaidi kuhusu historia ya Utalii wa Puto katika Utalii.

Utalii wa puto (hot air ballooning) ni mojawapo ya aina ya utalii inayohusisha kuruka na kutazama mandhari mbalimbali kutoka angani kwa kutumia puto inayotumia moto. 

Ikumbukwe kuwa historia ya utalii huu inaanzia karne ya 18, baada ya kubuniwa kwa mara ya kwanza na Wafaransa, ndugu Joseph-Michel na Jacques-Étienne Montgolfier mwaka 1783.

 Kabla ya kuanza lilifanyoka jaribio la kwanza la kurusha puto iliyotumia hewa ya moto, na hatua hii ilifungua milango kwa maendeleo ya safari za anga.

Hivyo  miaka iliyofuatabutalii wa puto ulianza kuvutia wapenzi wa mandhari na wapenzi wa mazingira, hususan maeneo ya asili na hifadhi za wanyama na mengine ndani ya Hifadhi Duniani.


Hivyo utalii huu ulianza kushika kasi zaidi katika karne ya 20, baada ya teknolojia ya puto kuboreshwa, ikiwapa watalii nafasi ya kutazama maeneo ya mbali na ya kuvutia.

 Kwa upande wa nchi kama Tanzania na  Kenya na  Afrika Kusini zilianza kuitumia huduma hii katika hifadhi zao za wanyama kama Serengeti na Masai Mara, ambapo watalii walianza kushuhudia wanyama pori kutoka angani.

Kutokana na mandhari yake ya kipekee, utalii wa puto umekuwa maarufu sana katika maeneo yenye hifadhi za wanyama, milima, na majangwa mfano Jangwa la Sahara na eneo la Cappadocia nchini Uturuki ni miongoni mwa maeneo maarufu kwa utalii huu.

Miaka ya hivi karibuni utalii wa puto umeongezeka katika maeneo mengi duniani, ukivutia watalii wanaopenda mandhari ya angani na wanyamapori. 

Kupitia Teknolojia bora zaidi na huduma zinazozingatia usalama zimechangia ukuaji wa sekta hii, na kufanya utalii wa puto kuwa moja ya njia bora za kuvutia watalii wa kimataifa na wa ndani.

Hivyo kwa picha hiyo fupi tunapata jibu sahihi kwanini utalii wa puto ni kivutio katika maadhimisho ya Miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Jinsi utalii huu utakavyovuta watalii zaidi Ruaha .

Wakati Hifadhi hii inakwenda kuadhimisha Miaka 60 toka ilipoanzishwa rasmi mwaka 1964 kutoka kwenye Pori la akiba la Saba wamekuja na ubunifu huo wa utalii wa puto kama nyenzo na Teknolojia mpya ya kuvutia watalii .

 Utalii huu unatarajiwa kutoa fursa kwa watalii kutazama mandhari ya kuvutia na makundi ya wanyama kama Nyati,simba, tembo, nyati, na pundamilia na wengine  kwa mtazamo wa kipekee ukiwa  angani kwenye Puto.


Mkuu wa Hifadhi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Godwell Ole Meing’ataki, ameeleza kuwa utalii huu utachochea maendeleo ya utalii ndani ya hifadhi na kuongeza idadi ya watalii, hivyo kuchangia mapato ya hifadhi na serikali.

Tofauti na utalii wa magari, utalii wa puto unatoa uzoefu wa pekee kwa watalii kushuhudia wanyama wakiwa katika makazi yao ya asili bila kuwavuruga. 

Kuwa utalii wa Puto utawapa watalii nafasi ya kuchukua picha na kujionea mazingira ya hifadhi kutoka juu. 

Pia utasaidia  kuvutia watalii zaidi na kuimarisha biashara zinazohusiana na utalii kama vile malazi, migahawa, na huduma za usafiri. 

" Utalii huu utachangia kuongezeka kwa mapato ya utalii kwa taifa kwa kuongeza ada zinazolipwa na wageni watakaotumia huduma hii"

Hata hivyo anasema wanaendelea na maandalizi na Shughuli za Maadhimisho hayo ya kihistoria ambayo yanaandika rekodi nzuri.


Maadhimisho hayo yatakuwa na shughuli mbalimbali zinazohusisha jamii, viongozi wa kimila, na viongozi wa dini.

Pia  ziara maalum ya kutembelea hifadhi itafanywa na Chifu wa Wahehe pamoja na viongozi wa kidini, lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano kati ya jamii na hifadhi.

 Kongamano maalum pia litaandaliwa kwa ajili ya kujadili mafanikio ya hifadhi, changamoto zilizopo, na mbinu bora za kuimarisha uhifadhi na utalii katika hifadhi hiyo.

Kuwa shughuli nyingine zitajumuisha elimu kwa watoto na vijana juu ya umuhimu wa uhifadhi wa maliasili, kwa lengo la kuandaa kizazi chenye uelewa wa masuala ya mazingira. 

Aidha kutakuwa na maonyesho ya biashara na bidhaa za asili zinazotokana na maliasili za hifadhi, kama njia ya kuchochea biashara na uchumi wa eneo hilo.


Ikumbukwe kuwa Hifadhi ya Ruaha ni chanzo kikuu cha mapato kwa mkoa wa Iringa na kwa taifa kupitia sekta ya utalii.

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Iringa mjini Frank Nyalusi anasema anaziona fursa lukuki kupitia maadhimisho ya Miaka 60 ya Hifadhi ya Ruaha .

Kwani anasema Kupitia Wageni wa ndani na  wa kimataifa na wa wanaolipa ada za kuingia, kutumia malazi, na huduma zingine huchangia kukuza uchumi wa Taifa na uchumi wa wakazi wa mkoa wa Iringa.

"Ukiacha kukuza Pato la Taifa Hifadhi pia inatoa ajira kwa wananchi wanaozunguka  Hifadhi hiyo ila hata nje ya maeneo ya jirani kwani mzunguko wake ni mnyororo mrefu zaidi kwa kupitia huduma za  biashara za kiutalii na nyingine wageni wanaopita huacha pesa"

Anasema maadhimisho hayo yaende Sanjari na ukamilishaji wa uwanja wa Ndege wa Iringa ambao upo hatua za Mwisho itawasaidia kufungua utalii wa kusini hususani Hifadhi ya Ruaha.

Pia Nyalusi anasema tayari anaona Mwanga wa kuanza ujenzi wa Barabara ya lami kati ya Iringa mjini kwenye Hifadhi ya Ruaha ambayo ikimalizika  itachangamsha utalii ndani ya Hifadhi hiyo .

Sarafino Lanzi ni mwongoza watalii ndani ya Hifadhi ya Ruaha kwa zaidi ya Miaka 20 sasa anasema kupitia maadhimisho hayo na uzinduzi wa utalii wa puto dhamani ya utalii inapongezwa zaidi .

Kuwa watalii wa Puto ambao walikuwa wakielekea Hifadhi ya Serengeti kufanya utalii wa puto sasa watafika Hifadhi ya Ruaha kutalii pia .

Pamoja na utalii, Hifadhi ya Ruaha inachangia uzalishaji wa nishati kwa taifa kupitia Mto Ruaha, ambao ni chanzo cha maji ya bwawa la Mtera, mojawapo ya vyanzo vikubwa vya umeme nchini Tanzania.

 Ni wazi uhifadhi wa mto huo una umuhimu mkubwa kwa uzalishaji wa nishati na ustawi wa taifa letu Tanzania na ndio maana wadau mbali mbali wamelekeza nguvu kutunza moto huo .

Kwani maadhimisho ya miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha yanabeba maana kubwa kwa uhifadhi na utalii nchini Tanzania.

" Uzinduzi wa utalii wa puto unatarajiwa kuvutia wageni wengi zaidi, na kuongeza mapato kwa hifadhi na uchumi wa mkoa wa Iringa." alisema Lanzi


Pamoja na maadhimisho haya bado Hifadhi ya Ruaha itaendelea kuwa nguzo muhimu ya uchumi na urithi wa asili wa Tanzania .

Na  maadhimisho haya ni fursa adhimu ya kusherehekea mafanikio makubwa ya hifadhi, kukuza mwamko wa jamii kuhusu uhifadhi, na kuimarisha sekta ya utalii kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA FRANCIS GODWIN MTAYARISHAJI WA MAUDHUI MATUKIO DAIMA MEDIA ANAPATIKANA KWA SIMU 0754026299 BARUA PEPE.matukiodaima3@gmail.com

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI