Kampuni ya Asas Group imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii mkoani Iringa kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo ya kijamii. Asas Group, chini ya uongozi wa mfanyabiashara na mwekezaji Salim Asas, imewekeza katika sekta muhimu kama vile afya, elimu, na miundombinu.
Mchango wa Asas katika Jamii
Moja ya maeneo makubwa ambapo Asas Group imechangia ni kuboresha huduma za afya. Kampuni hiyo imetoa misaada ya vifaa tiba kwa hospitali za mkoa wa Iringa na ujenzi wa wodi , jambo ambalo limeimarisha huduma za afya kwa wananchi. Pia, imekuwa ikisaidia sekta ya elimu kwa kutoa vifaa vya shule na kuchangia ujenzi wa madarasa katika shule za vijijini, hatua inayosaidia kuinua kiwango cha elimu.
Katika sekta ya miundombinu, Asas Group imesaidia Miundo mbinu ya barabara ili kurahisisha usafiri wa bidhaa na huduma kwa wananchi wa Iringa. Pia, wamejikita katika kusaidia wafugaji kufunga Kisasa zaidi hivyo kuchochea maendeleo ya ufugaji na kuinua kipato cha wananchi.
Ikumbukwe kupitia mchango wake katika sekta mbalimbali, Kampuni ya Asas Group imejijengea heshima na imani kubwa mkoani Iringa kwa kuonyesha nia ya dhati ya kuboresha maisha ya jamii, huku ikileta maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Moyo wa kujitolea wa kampuni hii ya kizalendo yenye makao yake makuu mjini Iringa ni mfano kwa makampuni mengine kuiga kuwekeza kwa jamii zaidi .
0 Comments