Header Ads Widget

HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIBAYA RIPOTI YA CAG ZAONYWA KUTORUDIA TENA

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU, Ludovick Utouh akiteta jambo la mkuu wa wilaya ya Iringa Khery James Leo wakati wa Mafunzo ya kuwajengea Uwezo wakurugenzi, maofisa manunuzi na Ugavi wa Halmashauri zilizofanya vibaya Ripoti ya CAG.

Na Matukio Daima App 

MKUU wa mkoa wa Iringa Peter Serukamba amewataka wakurugenzi na Wakuu wa vitengo vya ununuzi na Ugavi wa halmashauri zilizofanya vibaya kwenye taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali nchini, (CAG) kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kubadilika.

Kuwa ili kuliletea Taifa maendeleo ni lazima wahusika wa manunuzi kwenye Halmashauri kufanya kazi hiyo kwa weledi zaidi ili Halmashauri zao zisijirudie kwa orodha mbaya ya  CAG ya kufanya vibaya.

Akifungua Mafunzo hayo leo katika ukumbi wa Sunset Hotel mjini Iringa,Serukamba ambae aliwakilishwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Khery James katikati ufunguzi wa Mafunzo ya kuwajengea Uwezo 

Wakurugenzi na Wakuu wa vitengo vya ununuzi na Ugavi wa Halmashauri zilizofanya vibaya Ripoti ya CAG.

Katika  mafunzo hayo yaliyoandaliwa na bodi ya wakurugenzi ya PSPTB kwa kushirikiana na taasisi ya Wajibu  (Institute of Public Accountability) alisema kuwa watumishi wa vitengo hivyo wanatakiwa  kusimamia sheria za manunuzi kwa kuzingatia misingi ya taaluma zao.

Hata hivyo alisema mafunzo hayo, yatawasaidia, maafisa ugavi kufanya manunuzi yenye tija kwenye halmashauri zao kama ambavyo sheria zinaelekeza.

"Nimeambiwa kuwa kwenye mafunzo haya tutapitishwa kwenye mabadiliko ya  sheria ya mwaka 2023 na utaratibu wa ununuzi wa kutumia mfumo mpya wa nest ambao unatumika sasa badala ya ule wa mwazo wa times" Alisema Dc Kheri James.

Aidha aliwataka waatalamu wa ununuzi na ugavi kufuatilia kwa makini mafunzo hayo, ili kupata uelewa zaidi, utakao wasaidia kufanya ununzi wenye tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

"Na hii ni nafasi ya pekee kwa maafisa masuhuri na wataalamu wa ununuzi wa ugavi kufuatilia kwa makini na kuelewa ili turudipo kwenye halmashaurini zetu tukafanye ununuzi wenye tija kwa taifa letu na wananchi wote kwani kufanya hivyo ni kuonyesha uadilifu wetu na kuzingatia misingi ya taaluma zetu" Alisema Dc Kheri James. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi, alisema lengo la mafunzo hayo nikuwajengea uwezo wakurugenzi na wakuu wa vitengo vya manunuzi kwa halmashauri thelathini ambazo zimeonekana kufanya vibaya kupitia taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali nchini (CAG).

"Nishukuru mwitikio wa viongozi hawa ambao ni wakurugenzi na wakuu wa vitengo vya manunuzi wa hamalshauri thelathini nchini (30) sisi kama bodi tunawajibu wa kuwaongezea uwezo (kudevelop) na kuhakikisha kwamba taaluma ya ununuzi na ugavi inafanya kazi ipasavyo na iweze kutoa mchango sahihi kwa nchi yetu, hasa ukizingatia serikali inatoa fedha nyingi sana na zinaelekezwa 

MKUU wa mkoa wa Iringa Peter Serukamba amewataka wakurugenzi na Wakuu wa vitengo vya ununuzi na Ugavi wa halmashauri zilizofanya vibaya kwenye taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali nchini, (CAG) kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kubadilika.

Kuwa ili kuliletea Taifa maendeleo ni lazima wahusika wa manunuzi kwenye Halmashauri kufanya kazi hiyo kwa weledi zaidi ili Halmashauri zao zisijirudie kwa orodha mbaya ya  CAG ya kufanya vibaya.

Akifungua Mafunzo hayo leo katika ukumbi wa Sunset Hotel mjini Iringa,Serukamba ambae aliwakilishwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Khery James katikati ufunguzi wa Mafunzo ya kuwajengea Uwezo 

Wakurugenzi na Wakuu wa vitengo vya ununuzi na Ugavi wa Halmashauri zilizofanya vibaya Ripoti ya CAG.

Katika  mafunzo hayo yaliyoandaliwa na bodi ya wakurugenzi ya PSPTB kwa kushirikiana na taasisi ya Wajibu  (Institute of Public Accountability) alisema kuwa watumishi wa vitengo hivyo wanatakiwa  kusimamia sheria za manunuzi kwa kuzingatia misingi ya taaluma zao.

Hata hivyo alisema mafunzo hayo, yatawasaidia, maafisa ugavi kufanya manunuzi yenye tija kwenye halmashauri zao kama ambavyo sheria zinaelekeza.

"Nimeambiwa kuwa kwenye mafunzo haya tutapitishwa kwenye mabadiliko ya  sheria ya mwaka 2023 na utaratibu wa ununuzi wa kutumia mfumo mpya wa nest ambao unatumika sasa badala ya ule wa mwazo wa times" Alisema Dc Kheri James.

Aidha aliwataka waatalamu wa ununuzi na ugavi kufuatilia kwa makini mafunzo hayo, ili kupata uelewa zaidi, utakao wasaidia kufanya ununzi wenye tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

"Na hii ni nafasi ya pekee kwa maafisa masuhuri na wataalamu wa ununuzi wa ugavi kufuatilia kwa makini na kuelewa ili turudipo kwenye halmashaurini zetu tukafanye ununuzi wenye tija kwa taifa letu na wananchi wote kwani kufanya hivyo ni kuonyesha uadilifu wetu na kuzingatia misingi ya taaluma zetu" Alisema Dc Kheri James. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi, alisema lengo la mafunzo hayo nikuwajengea uwezo wakurugenzi na wakuu wa vitengo vya manunuzi kwa halmashauri thelathini ambazo zimeonekana kufanya vibaya kupitia taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali nchini (CAG).

"Nishukuru mwitikio wa viongozi hawa ambao ni wakurugenzi na wakuu wa vitengo vya manunuzi wa hamalshauri thelathini nchini (30) sisi kama bodi tunawajibu wa kuwaongezea uwezo (kudevelop) na kuhakikisha kwamba taaluma ya ununuzi na ugavi inafanya kazi ipasavyo na iweze kutoa mchango sahihi kwa nchi yetu, hasa ukizingatia serikali inatoa fedha nyingi sana na zinaelekezwa kwaajili ya maendeleo ya wananchi. alisema Mbanyi.

Mbanyi alisema kupitia mafunzo hayo watapata nafasi ya kujua eneo lenye changamoto kwa halmashauri husika na namna ya kuweka mikakati ya pamoja ya kutatua changamoto hizo.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU, Ludovick Utouh, alisema uchaguzi wa halmashauri hizo thelathini umetokana na kuangalia zile ambazo zinakabiliwa na matatizo makubwa zaidi hasa katika upande wa manunuzi.

 Taarifa za CAG hutolewa kwa lengo la kusaidia serikali na wananchi kwa ujumla na siyo kwa lengo lingine kama ambavyo baadhi ya watu wanavyofikiria na iwapo kuna halmashauri inaona kunautofauti inaruhusiwa kutembelea ofisi za CAG ili kupata maelezo zaidi.

"CAG amepewa majuku makubwa kwa kuwa yeye ndiyo jicho la wananchi linapokuja rasilimali zao, hivyo mapendekezo ya CAG yanalenga katika kuasaidia, zaidi ya yote kumsaidia Accounting officer ambaye ndiyo DED kufanya majukumu yake vizuri, na ukiwa mkurugenzi hakikisha hoja zilizoibuliwa zinatekelezwa na kama utakwama ofisi ya CAG iko wazi muda wote, piga simu au nenda mtapata matokeo mazuri, Alisema CAG Msastaafu Ludovick Utouh.

Mkufunzi wa mafunzo  hayo Amos Kazinza aliwakumbusha wakurugenzi na wakuu hao wa ununuzi kutumia mfumo mpya wa nest katika kufanya ununuzi wa serikali, ili kuweza kuwa na kuweka kumbukumbu na kuwa taarifa sahihi za ununuzi. 

Pia aliwakumbusha sheria zinazoweza kuwakabili wataalamu hao, pindi watakapobainika kwenda kinyume na sheria za kufanya manunuzi ya serikali kupitia mfumo wa nest ikiwemo kulipa faini ya shilingi milioni 10, kifungo kisicho pungua miaka mitatu ama vyote kwa pamoja.

Post a Comment

0 Comments

MAGAZETI

NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI