Na Matukio Daima Media, Dar es Salaam
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi (CDF),Jenerali John Mkunda kupitia uratibu wa baraza la michezo la majeshi ya ulinzi Dunia( conseil International du sports Military) imewaleta wakufunzi na wataalum kutoa mafunzo ya makocha, lengo ni kuwaaendeleza maofisa na askari wenye taaluma ya ukocha wa mpira wa miguu kuunga mahusiano mazuri yaliyofanywa kati ya Tanzania na Nedharland.
Aidha dhamira ya CDF ni kupata walimu wazuri watakao saidia timu za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zinazoshiriki ligi mbalimbali nchini na za Taifa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti makocha ambao ni maofsa wa JWTZ na askari wamemshukuru CDF kwa kuona umuhimu wa mafunzo hayo kwa makocha na kwamba wakufunzi wa TFF wamekuwa wakitoa mafunzo mbalimbali lakini walimu hapo wakigeni wana ujuzi zaidi na vifaa hivyo wanatoa ahadi ya kufanya vizuri katika kuhakikisha timu za majeshi na Taifa zinafanya vizuri.
Mafunzo haya ni ya wiki mbili na ijumaa jioni yatafungwa rasmi hii inatokana na mahusiano mazuri ya Chama Cha Mpira wa miguu Cha majeshi .
Mwisho
0 Comments