Josaya Luoga Katibu mwenezi CCM mkoa wa Njombe
Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP Njombe
Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe kimewaagiza wakuu wa Taasisi zote za Serikali kuhakikisha wanakwenda kukamilisha miradi ambayo haijakamilika hadi sasa ili kuondoa kero zinazoibuka kwa wananchi mara kwa mara.
Katika Majumuisho ya Masuala yaliyojadiliwa ndani ya Mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Njombe Katibu wa Itikadi,Siasa Uenezi na Mafunzo mkoa Josaya Luoga amesema Chama hicho hakitaki kusikia kero na Malalamiko ya wananchi yakiendelea kusikika juu ya mkwamo wa miradi mbalimbali ili hali serikali inapeleka fedha za maendeleo.
Aidha wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali akiwemo Meneja wa NFRA Kanda ya Makambako Revocatus Bisima amesema tayari zaidi ya Tani elfu 18 za mahindi zimeshanunuliwa toka kwa wakulima.
Kwa upande wa miradi ya Maji inatajwa kufikia asilimia 86 katika utekelezaji wake katika maeneo ya Vijijini.
Mhandisi Costantine Ibengwe ni Kaimu meneja wa Wakala wa Barabara mijini na Vijijini TARURA Mkoa wa Njombe ambaye mbali na mafanikio Lukuki ya Utekelezaji wa miradi hiyo kufanyika lakini anakiomba chama cha mapinduzi CCM Kupitia viongozi wake kusaidia katika utatuzi wa baadhi ya Changamoto.
Naye Ofisa Kilimo mkoa wa Njombe Wilson Joel anaweka wazi mchakato wa upatikanaji wa pembejeo za ruzuku za kilimo katika msimu mpya wa Kilimo ujao na kwamba safari hii Kila Halmashauri itakuwa na Vituo vitatu vya mawakala wakubwa vya kupata pembejeo hizo.
Kwa upande wake Katibu tawala mkoa wa Njombe Judica Omary Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa anasema serikali imeendelea kuleta Mabilioni ya Fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo.
Changamoto za mkwamo wa ujenzi wa miundombinu ya barabara kwenye baadhi ya maeneo mkoani Njombe ni miongoni mwa mambo yanayohimizwa kufanyiwa kazi kabla mvua hazijaanza kwani zitakatisha mawasiliano na hata uchumi.
0 Comments