NA WILLIUM PAUL, DODOMA.
MABINGWA wa kombe la Mkenda cup timu ya Rongai FC imeshirika kikao cha Bunge jijini Dodoma ikiwa ni ahadi ya Mbunge wa Jimbo la Rombo na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda bingwa wa michuano kualikwa Bungeni.
Timu hiyo iliibuka kidedea baada ya kuifunga timu ya Kelamfua mokala kwa mikwaji ya penati 4 kwa 3 baada ya kwenda droo ya goli moja kwa moja dakika tisini.
Michuano hiyo ya Mkenda cup imekuwa na ushindani mkubwa mwaka hadi mwaka ambapo mwaka huu timu 123 zilishiriki.
Bingwa huyo anatarajiwa jioni ya leo kucheza mechi na timu ya Fountain Gate high school katika viwanja vya Fountain gate arena jijini Dodoma.
Mwisho.
0 Comments