Header Ads Widget

BARAZA LA MADIWANI LAWATAKA WATENDAJI WA KATA KUWAJIBIKA

 






Madiwani wa halmashauri ya wilaya Nkasi wametakiwa kuongeza nguvu ya usimamizi Kwa Maafisa Watendaji wa kata zao kuhakikisha kwamba Kasi ya ukusanyaji wa mapato inaongezeka.


Hayo Yamejili Leo septemba 04,2024 katika baraza la madiwani la Robo ya mwaka wa fedha 2024/2025 yamesemwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Nkasi Pankrasi Maliyatabu kwenye kikao Cha Baraza la Madiwani Leo ambapo amedai kuwa Moja ya jukumu lao kubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ni pamoja na suala la Zima la kuhakikisha katika maeneo Yao makusanyo ya halmashauri yanapatikana.


Amedai kuwa Ili halmashauri iweze kupata uwezo wa kushughulika na uendelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo Yao ni lazima fedha iwepo na hili kuweza kufanikisha katika Hilo ni lazima kuwepo na makusanyo,hivyo ni lazima kila Mmoja aone kwamba ukusanyaji wa mapato ni jukumu lake Kwa kuwasimamia na kutoa ushirikiano wa kutosha Kwa Watendaji wao.


Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Hafra Nassoro Kwa upande wake amedai kuwa suala la upotevu wa mapato Kwa Watendaji wa kata amelipata na kuwa kufuatia hari hiyo akizungumza nao na na kuwekeana mikakati na kuwa Sasa kila mwisho wiki kila Mtendaji wa kata atakua anatoa taarifa ya mapato katika kata yake.


Amesema kuwa  pia ataendelea kufanya vikao na Maafisa Watendaji wa kata vya mara Kwa mara Ili kuhakikisha kwamba mapato yanapatikana katika maeneo Yao na kuwezesha halmashauri kufikia malengo ya makusanyo na hata ikibidi kuvuka lengo.


Awali afisa serikali za mitaa mkoani Rukwa Vaileth Shirima Kwa upande wake amewataka Madiwani na Watendaji wa halmashauri kuhakikisha kwamba wanatoa ushirikiano wa kutosha Kwa mkurugenzi mtendaji ambaye ni mgeni na kuwa hiyo ndiyo itakuwa jawabu la kuyafikia maendeleo wayatakayo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI