Header Ads Widget

WIZARA YA NISHATI KUTUMIA MAONESHO YA NANENANE KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA




Na Hamida Ramadhani matukio Dodoma App Dodoma

KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesm Mramba, amesema maonesho ya nanenane watayatumia kuhamasisha wanachi matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo matumizi ya gesi itokanayo na kinyesi cha mifugo.


Mramba, alisema hayo leo jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya wakulima kitaifa yanayofanyika viwanja vya Nzuguni jijini hapa.


"Tunakwenda kuhamasisha watu wenye mifugo kuanza kutumia nishati itokanayo na kinesiology cha mifugo hata kama mtu na ng'ombe wawili basi hao watumike kuzalisaha nisahti Safi ya kupikia"amesema


Vile vile, alisema tayari wamendaa mkakati wa kuelisha jamii uhumuhimu wa matumizi ya nisahati safi ya kupikia ambao utekelezaji wake unaanza mwezi huu mwishoni.


"Kupitia mkakati huu tunakwenda kutoa elimu kwa umma pamoja na kugawa mitungi ya gesi ya kupikia na tayari wakala wa nisahti vijijini (REA) tayari wameshaingia makubaliano na Magereza yote nchini kuwafungia mitungi ya gesi ya kupikia"amesema


Katika hatua nyongine Katibu huyo amesema kama wizara wapo katika hatua za mwisho wa mazungumzo na wadau ili kuanza usalisahji wa mbolea kwa kutumia gesi asilia.


Amesema wao kama wizara ya Nishati ni wadau wakubwa katika kuwezesha shughuli za kilimo na mifugi nchini.


Ameeleza, uzalishaji huo ukianza utasaidia wakilima kupata mbole kwa gharama nafuu na kuipunguzia mzigo serikali kuagiza nje ya nchi.


Aidha, amesema wizara ya nishati imeshiriki maonesho hayo kutokana na kuwa na jukumu kubwa la kupeleka huduma za umeme kwenye miradi ya umwagiliaji pamoja na viwanda video vya kilimo.


"Lakini pia hivi sasa tunafanya jihad kuongeza upatikanani wa gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya vyombo vya moto ili kuwezesha kurahisisha usafirishaji wa mazo ya kilimo na mifugo.


"Sasahivi magari ya Kampuni ya Dangote ndiyo yanatumia gesi asili lakini na sisi kama serikali tunafanya jitihada za makusudi kuingeza upatikanaji wa gesi hii kwa ajili ya matumizi ya vyombo vya moto ili kurahisisha usafirishaji wa mazao ya kilimo na mifugo"alalisemmesema



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI