Header Ads Widget

WANANCHI WA MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WAENDELEA KUPATIWA ELIMU YA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI,NANENANE ARUSHA



Na,Jusline Marco;Arusha

Bodi ya Maji Bonde la Pangani Kanda ya Kaskazini imeungana na viongozi wa Mkoa wa Arusha kuhakikisha inatoa elimu kwa wananchi wanaofika katika maonesho ya Nanenane kuhusiana na kazi ambazo zinafanywa na bodi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 30 ya Kilimo na Sherehe za Nanenane 2024 yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro Jijini Arusha,Mkurugenzi wa Bodi hiyo Bwn.Segule Segule amesema,lengo  kubwa la Bodi hiyo ni usimamizi wa rasilimali maji.

Bwn.Segule ameongeza kuwa wakati umefika kwa wananchi kufahamu umuhimu wa mita 60 katika kuhiadhi vyanzo vya maji ambapo amesema kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo maonesho hayo elimu kwa wananchi inaendelea kutolewa.

Kwa upande wake Mtaalamu wa Maji juu ya Ardhi Brown Mwangoka amesema lengo kuu la ushiriki wao ni kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na masuala ya kuhifadhi,kutunza na kulinda vyanzo vya maji kwa shughuli za upandaji wa miti rafiki na maji na uwekaji wa alama za mipaka katika maeneo ya vyanzo vya maji.

Maonesho ya 30 ya Kilimo na Sherehe za Nanenane 2024 Kanda ya Kaskazini yanafanyika kwa kaulimbiu ya Chagua viongozi bora wa serikali za mitaa kwa maendeleo ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi ambapo Kitaifa maonesho hayo yanafanyika jijini Dodoma.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI