Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe.Dk.Linda Salekwa akiongoza kikao cha mapitio ya maktaba wa lishe ngazi ya kata,Mitaa na vijiji robo ya nne ya mwaka 2023/2024 .
Baadhi ya maafisa lishe na Maafisa Watendaji Kata wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe.Dr.Linda Salekwa.
Baadhi mazao ya vyakula vinavyo hitajika kutumiwa na Wanafunzi mashule kama Maharage na mahindi .
**************
Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP Mufindi.
WANANCHI na Wazazi wa Wanafunzi wanaosoma Shule katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, kutumia fursa ya kipindi cha mavuno kupeleka Chakula shuleni.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Dr..Linda Salekwa katika kikao cha mapitio ya mkataba wa lishe ngazi ya kata,Mitaa na vijiji robo ya nne ya mwaka 2023/2024 kilichofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Mhe.Dr.Salekwa amesema takwimu zinaonyesha kuwa baadhi ya kata zipo chini ya asilimia 60 hii inaonyesha Kuna Wanafunzi hawapati Chakula shuleni.
"Maafisa nashauri kuhakikisha kuwa Wananchi wanatumia fursa hii ya kipindi cha mavuno kupeleka Chakula shuleni" Alisema DKT.Salekwa .
Upande wake Afisa lishe wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bw.Salumu Atlas alisema mashindano ya siku za Vijiji lengo lake ni kuhamasisha masuala ya lishe ya Kijiji na kuepukana na udumavu kwa Jamii .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi.Fedelica Myovella amesema Halmashauri ya Mji Mafinga imejipanga kuwatambua Wanaofanya vizuri kwenye Kata zao na kuonyesha mafanikio na matokeo chanya.
Bi.Myovella alisema Halmashauri inatarajia kuandaa mashindano ya siku za vijiji lengo likiwa ni kuhamasisha masuala ya lishe kwa kina Mama Wajawazito na Wanaonyosha.
Aidha kikao hicho kiliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe.Dr.Salekwa na kuhudhuriwa na Wakuu wa idara na Maafisa Watendaji kutoka katika Kata.
0 Comments