Washiriki zaidi ya elfu moja wanatarajia kushiriki tamasha la tukacharu forest linalotarajia kufanyika tarehe 24 na 25 mwezib katika msitu wa rau uliopo Moshi moshi mkoani Kilimanjaro .
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo mkuu wa wilaya ya Moshi zephania Sumaye amese malengo mahususi ya tamasha hilo ni kutangaza utalii wa ndani kutokana na Kilimanjaro kubarikiwa kuwa na vivutio vingi ikiwemo msitu huo ambao upo katikati ya mji wa moshi.
"Mstu huu upo katikati ya mji kabisa lakini kwa jinsi ulivyohifadhiwa uanapokuwa ndani unaweza usijue kuwa upo ndani ya mji "Alisema.
Amesema kuwa katika msitu huo unapatikana vivutio vingi vya kitalii kuanzia mandari maeneo ya picnic na mti mrefu kuliko yote barani Afrika pamoja na mbega wenye rangi nyeupe.
" tarehe 24 tutaanza na mazoezi ya kukimbia na kwa wale ambao hawawezi kukumbia watatembe na baada ya hapo tutatoa medali na zawadi kwa washindi.
Kwa upande wa Mhifadhi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Moshi, Godson Ulomi amesema Tukacharu mwaka huu imeboreshwa zaidi ikilinganishwa na mwaka jana ambapo kutakuwa na mashindano ya mbio za baiskeli Kilometa 75, kukimbia kilometa tano na 21 pamoja na matembezi ndani ya msitu huo.
"Tukacharu awamu ya kwanza ilifanyika mwaka jana na hatua hiyo iliongeza idadi ya watalii katika msitu wa Rau na kwa mwaka huu tumeboresha zaidi ambapo mashindano ya baiskeli, kukimbia na matembezi ndani ya msitu"alisema Ulomi
Mratibu wa tukacharu Rau forest amesema kuwa washiriki watakaoshiriki tukacharu rau forest watapewa zawadi na medali .
0 Comments