Header Ads Widget

MCHENGERWA AMTUMBUA DMO, AAGIZA TAKUKURU KUFANYA UCHUNGUZI KWENYE MIRADI

 

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa (kushoto)  akiwa na Mganga Mkuu wa halmashauri ya mji wa Kasulu Peter Janga (kulia) ambaye ameamriwa kuondolewa kwenye halmashauri hiyo

Na Fadhili Abdallah,Kigoma


Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na serikali za mitaa, Mohamed Mchengerwa amenusa harufu ya matumizi mabaya ya fedha katika miradi ya elimu na afya wilayani Kasulu mkoani Kigoma na kuagiza kuondolewa kwenye nafasi yake kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Kasulu huku akiagiza kufanyika kwa uchunguzi  wa matumizi ya fedh katika mradi wa sekondari mpya ya Rungwe mpya.

Waziri Mchengerwa ametoa maaagizo hayo akiwa kwenye siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu mkoani Kigoma ambapo ameonesha kusikitishwa na kusuasua kwa utekelezaji wa miradi hiyo huku serikali ikiwa imetoa kiasi kikubwa cha pesa ambapo miradi hiyo inashindwa kukamilika kwa wakati lakini kukiwa na dalili za matumizi mabaya ya fedha kwenye miradi hiyo.

Akiwa kwenye kituo kipya cha afya cha Mwami Ntare wilayani Kasulu Waziri Mchengerwa alishuhudia kuanza kutoa huduma kwa kituo hicho kwa karibu mwaka sasa lakini kukiwa hakuna samani kwa ajili ya watoa huduma na wagonjwa huku Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji wa Kasulu, Peter  Janga akishindwa kutoa maelezo ya kueleka sababu inayofanya kituo kutokuwa na samani hizo na hivyo kuangiza kuondolewa kwa Mganga huyo wa wilaya kwenye wadhifa wake.

Sambamba na maagizo hayo akiwa wilayani  Kasulu Waziri wa TAMISEMI alitembelea shule ya Sekondari Rungwe Mpya ambapo taarifa ya utekelezaji wa mradi huo ilimtia shaka Waziri kuhusu uadilifu wa matumizi ya fedha na kuagiza TAKUKURU kufanya  uchunguzi wa matumizi ya fedha zilizotekeleza mradi huo.

Awali Mkuu wa shule hiyo, Paul Mkuyu  akitoa taarifa za utekelezaji kwa Waziri Mchengerwa alisema kuwa katika kiasi hicho cha shilingi Bilioni moja walijenga madarasa 13, jengo la utawala, nyumba mbili za walimu ambavyo vimekamilika ambapo hata hivyo mabweni manne ya wanafunzi, Jengo la chakula na baadhi ya majengo yakiwa hayajakamilika.


Alisema kuwa kupanda kwa gharama ya vifaa, mvua nyingi ni miongoni mwa sababu zilizochangia kuchelewa kukamilika kwa mradi huo na kuongezeka kwa gharama za vifaa ambapo inabidi wapate fedha nyingine kumalizia mradi huo.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI