Header Ads Widget

WANANCHI FIKENI BANDA LA BRELA KUSAJILI BIASHARA NA LESENI



Na Hamida Ramadhani matukio App Dodoma


WANANCHI wa Mkoa wa Dodoma pamoja na viunga vyake  wametakiwa kutembelea katika viwanja vya maonesho ya kilimo nanenane hususani katika  banda la Wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA) kwa ajili kupata uelewa juu ya umuhimu wa kusajili bidhaa zao.


Ameeleza kuwa wananchi wanaweza kutatuliwa changamoto zao pamoja kupatiwa elimu sahihi pale ambapo watafika katika banda hilo kwa lengo la kujengewa uwezo na kupata huduma ya usajili wa bidhaa zao na kwa kuziongezea ubora bidhaa hizo.


 Akizumgumza na wananchi na waandishi wa habari Afisa Kumbumbukumbu BRELA,Farid hoza amesema  mwananchi akifika katika banda hilo watapata uelewa zaidi juu ya umuhimu wa kusajili bidhaa ambazo wanazizalisha na kuziongezea ubora kwa kiwango kinachokubalika.


"Tunawasaidia  wanawasaidia wakulima, wafanyabishara kuweza kufanya maombi yao ya usajili. 


" Katika haya maonesho tunafanya usajili wa papo kwa papo kitu ambacho sio rahisi na kama ulikuwa na changamoto ya muda mrefu haitatuliki ukija kwenye banda letu la Brela tunakusaidia Baraka, " Amesema


Na kuongeza " Tunatoa elimu kitu ambacho unaweza usikipate ukiwa nyumbani lakini ukija hapa tunakupa elimu, " Amesema Afisa kumbukumbu huyo. 


Pia amesema kwamba kutokana na umuhimu wa kujisajili wamekuwa wakitembea mikoani mbalimbali kutoa elimu ambapo mpaka sasa wanufaika niwengi kwani wameshatembea  takribani mikoa yote ya Tanzania pamoja na kuwafikia  wakulima na wafanyabishara na bado wanaendelea kwani zoezi hilo ni endelevu. 


Mpaka sasa waneshasajili makampuni zaidi ya 50 kwenye maonesho hayo ya nanenane. 


"Wito wananchi kuudhuria katika maonesho ili kusajili biashara zao unaposajili unatambulika kisheria


Wapo kwenye maonesho ya kimatifa ya kilimo yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni ambapo wapo kutoa huduma za usajili wa majina ya biashara, usajili wa makampuni,usajili wa alama za bishara na usajili wa Ataza na usajili wa leseni kundi A 


Mmoja wa wateja wa BRELA,Yahaya Hassan amefika katioa banda hilo  kufuatilia taarifa za kampuni yake huku akikiri kuwa kapata  huduma nzuri na  kuhudumiwa kwa haraka. 


"Huduma nzuri nimefurahi kwani nisingekuja hapa kwenye maonesho ingenilazimu kusubiri kwa muda wa siku tatu kwakuwa timu ya Brela iko hapa kila kitu inamalizwa hapa. 


Nashauri wote wenye changamoto ya makampuni, au majina ya biashara nivyema kusongea kwenye banda la Brela ili wapate huduma kwa haraka"amesema.

 

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI