Header Ads Widget

WANANCHI CHOME KUACHANA NA ZAO LA MIRUNGI.



NA WILLIUM PAUL, SAME. 


BAADHI ya wakazi wa Kata ya Chome wilayani Same mkoani Kilimanjaro waliokuwa wanajishughulisha na kilimo cha zao haramu la Dawa za kulevya jamii ya Mirungi wameondokana na kilimo hicho, hii ni baada ya Serikali kupitia Mfuko wa hifadhi ya milima ya tao la mashariki (EAMCEF) kuwawezesha miradi midogo midogo ya zao la Parachichi za kisasa.



Akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja Wilayani Same Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dustan Kitandula amesema ili miradi hiyo iweze kuwa na tija zaidi kwa wananchi hao ni vyema wakawezeshwa miradi mikubwa ambayo itasaidia pia kudhibiti shughuli za kibinadamu zinazo pelekea uharibifu wa Mazingira kwenye hifadhi za Taifa ikiwemo hifadhi ya msitu asilia Chome. 



Alisema kwa miaka kadhaa nyuma hifadhi hiyo ya asilia ilikumbwa na changamoto ya uvamizi wa shughuli za kibinadamu na kupelekea baadhi ya eneo la msitu kuharibiwa.


“Nimefurahi mradi huu ulivyopokelewa na wakazi wa Chome pamoja na kwamba tumeanza na kiwango kidogo lakini kuupokea kwa jinsi mlivyoupokea mmetupa matumaini, mmetupa changamoto ya kwenda kujipanga zaidi ili tulete miradi mikubwa zaidi hongereni sana”, Alisema Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dustan Kitandula.



Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Kasilda Mgeni amesema jumla ya miradi nane ya uhifadhi wa Mazingira kwa jaimii zinazo zunguka hifadhi za Taifa inatekelezwa Wilayani humo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni Hamsini na tatu (53) ikiwemo mradi wa miche ya Parachichi za kisasa zaidi ya mia tatu (300) uliopo Kata ya Chome, na kusisitiza kuwa Serikali ya Wilaya imejipanga kikamilifu kusimamia kwa karibu miradi hiyo ili iweze kuwa na tija kwa wanufaika lakini pia isaidie kwaajili ya uhifadhi wa Mazingira.



Francis Sabuni ambaye ni Mkurugenzi Mfuko wa hifadhi ya milima ya tao la mashariki (EAMCEF) amesema kwa kiasi kikubwa kulikotekelezwa miradi ya namna hiyo sehemu mbalimbali kwa jamii zinazo zunguka hifadhi za Taifa changamoto ya uharibifu wa mazingira yake imepungua na Mazingira ya hifadhi yameimalika ikiwemo hifadhi ya msitu asilia Chome lakini pia hata uchumi wa jamii hizo nao umeboreka.



Kata ya Chome ni moja ya eneo Wilayani Same kwamujibu wao watalaam wa kilimo wanaeleza zao la Parachichi limeonekana kustawi vizuri na kuwa na tija kwa wakulima hii ni kutokana na hali ya hewa ya eneo hilo kuwa ya bari na unyevu unyevu ikilinganishwa na Mikoa ya nyanda za Kusini inayosifika kwa kilimo cha zao hilo ikiwemo Mkoa wa Njombe.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI