Header Ads Widget

WAKULIMA NA WAFUGAJI MIKOA YA KANDA YA MASHARIKI HAWANA SABABU YA KUSHINDWA KUONGEZA TIJA

 


Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Balozi Dk Batrida Buriani,kulia,akianeshwa baadhi ya miti inayotumika kama dawa na mmoja wa maafisa wa Manispaa ya Morogoro kulia,alipotembelea Maonesho ya Wakulima na  Wafugaji Kanda ya Mashariki kaika,viwanja vya Mwalimu Julius  Nyerere mjini Morogoro.


Na Ashton Balaigwa,MOROGORO

WAKULIMA, Wafugaji  na Wavuvi walipo kaika Mikoa inayounda Kanda ya Mashariki ambayo ni Morogoro,Tanga,Dar es Salaam na Pwani wamelezwa hawana kisingizio wa la sababu ya kundishwa kufanya  vizuri kwenye sekta hizo kwakuwa mikoa hiyo imebalikiwa kuwa na Taasisi kubwa za Sekta hizo .

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Balozi Dk Batlida Buriani,alisema hayo wakati akifungua Maonesho ya wakulima,wafugaji na wavuvi katika mikoa ya kanda ya mashariki maarufu kama Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo Mkoani Morogoro.

Balozi Dk Batlida,alisema litakuwa ni jambo la ajabu kwa makundi hayo kushindwa kufanya vizuri wakati  katika sekta ya kilimo Mkoa kwa Morogoro kuna  Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA)pamoja na Taasisi mbalimbali za Utafiti wa Kilimo zipo na kwamba endapo wakulima wataweza kuvitumia kikamilifu  wataongeza uzalishaji na tija na hivyo kulingizia taifa mapato.

“ SUA wapo hapa  Morogoro,wamekuwa wakitoa mchango mkubwa sana katika sekta ya kilimo,hivyo wakulima wakija katika Maonesho haya watafaidika na kila elimu wanayotaka kuhusu kilimo hivyo hakuna sababu ya sisi Mikoa ya Kanda ya Mashariki kushindwa kufanya vizuri” alisema Balozi Batlida.

Kuhusu sekta ya Mifugo,Balozi Dk Batlida,alisema kwenye  Mkoa wa Tanga ipo Taasisi  ya Kitaifa ya Mifugo (TARIRI)ambayo wafugaji wa kanda hiyo ya Mashariki  wana uwezo wa kuitumia kwaajili ya kuboresha mifugo yao ikiwemo kunenepesha na kufuga kisasa.

Akizungumzia kuhusu seka ya Uvuvi,alisema kwa Mkoa wa Dar es Salaam ipo Taaisisi ya Utafiti wa Samaki na Uvuvi ambayo imekuwa ikitoa mchango mkubwa kuimarisha sekta hiyo hivyo hakuna sababu kwa sekta hivyo kushindwa kufanya vizuri.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Tanga,alisema asilimia 65 ya Watanzania kwa sasa wapo kwenye sekta hizo tatu za kilimo,mifugo na uvuvi ambayo wanachangia pato la Taifa asilimia 28 kutokana na bidhaa wanazozalisha  asilimia 24 kuuzwa nje ya nchi.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa wa Tanga,alisema maonesho hayo kila mwaka yamekuwa yakiimarika kuokana na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaotembelea kwaajili ya kujifunza teknolojia mbalimbali za Kilimo,Ufugaji na Uvuvi.

Alisema katika kipindi cha mwaka 2023 watu 75,000 walitembelea maonesho hayo na mwaka huu wanategemea yatatembelewa na watu zaidi ya 80,000 huku idadi ya washiriki  ikiongezeka kutoka watu 589 mwaka 2023 na kufikia 596 mwaka 2024.

Awali akisoma Taarifa ya Maonesho ya Kanda ya Mashariki,kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele,alisema lengo lake ni kutoa elimu kuhusu masuala ya kilimo,ufugaji na uvuvi ili waweze kujifunza mbinu mbalimbali za kuongeza tija.

Meja Gowele,alisema kupitia elimu hizo zitakazototolewa kwenye Maonesho hayo makundi hayo matatu yataweza kupata uvumbuzi wa kutatatua changamoto zao sambamba na kuongeza tija na hivyo kutoa mchango mkubwa kwa Taifa kupitia sekta hizo.

Mwisho.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI