Header Ads Widget

VIJANA CHADEMA WAONYA ATAKAYEHUJUMU CHAGUZI 2024/2025.

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Mratibu wa vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA (BAVICHA) Taifa Twaha Mwaipaya, amesema Chama Cha Mapinduzi kimechoka kuwaongoza wananchi ndio maana maisha ya wananchi yanaendelea kuwa magumu.


Mwaipaya amesema Chama hicho tawala kwa sasa kina viongozi wasio na maono ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwa pia na viongozi wengi wa kupita bila kupingwa hivyo kukosa uhalali wa kuwatumikia na kuwatetea wananchi.

Amesema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha maandalizi ya siku ya vijana ambayo kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani Mbeya ikiwa amefanya vikao katika kata za Nsalaga na Nzovwe jijini humo.


Amesikika akisema CHADEMA pamoja na wananchi wamechoka kuongoza na CCM kwani kwa zaidi ya miaka sitini bado wananchi wanaghubikwa na ufukara, hali ngumu ya maisha, haki za watu kuminywa na vitendo mbalimbali vilivyo kinyume cha haki za binadamu.


Hata hivyo katibu mwenezi huyo wa BAVICHA amewataka wana-Chadema na wananchi kwa ujumla kwenda kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kuchagua viongozi bora kwenye uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwakani huku akionya wasimamizi watakaohujumu matokeo kwenye chaguzi hizo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Vijana hao mkoa wa Mbeya Evaristo Elisha Chonya, amewataka wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi siku ya vijana ili kutafakari kwa pamoja mchango wa vijana na namna ya kusonga mbele kimaendeleo kupitia kundi hilo muhimu la vijana.


Chonya amesema CHADEMA haitavumilia kuona viongozi wa vyama vingine wanapita bila kupingwa bali mgombea atakayeshinda akatangazwe kwa haki bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Katibu wa CHADEMA mkoa wa Mbeya Hamadi Mbeyale amesema wakati wa mabadiliko ni sasa hivyo kuwaomba wananchi kuichagua CHADEMA kwenye chaguzi zijazo ili kuwa na viongozi wenye hofu ya Mungu na weledi katika kuwawakilisha na kuwatumikia wananchi badala ya kuwa na viongozi wanaotazama maslahi yao binafsi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI