Header Ads Widget

TARURA PWANI WAINGIA MIKATABA YA BARABARA NA WAKANDARASI

 


MKOA wa Pwani umeingia mikataba ya ujenzi wa barabara na wakandarasi yenye thamani ya shilingi bilioni 31.4 kupitia Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025.


Akisimamia usainiwaji wa mikataba ya ujenzi wa barabara wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba hiyo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema kuwa wanamshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya miundombinu ya barabara.


Kunenge alisema kuwa ili kuwe na uchumi na maendeleo ya kijamii lazima nchi ifunguke na shughuli ziweze kufanyika kwa wakati na kwa gharama nafuu hivyo ilani ya CCM imetekelezwa vizuri.


Naye meneja wa Tarura Mkoa wa Pwani  Mhandisi Leopold Runji alisema kuwa mbali ya kupatiwa kiasi hicho pia watapokea fedha kiasi cha shilingi bilioni 18 ambazo ni za ujenzi kwenye maeneo yaliyoathiriwa na mvua na kimbunga.


Runji alisema kuwa lengo la Tarura ni kuhakikisha

kuwa mikataba yote itakayosainiwa na wakandarasi waliosaini mikataba wanaenda kuanza utekelezaiji wa kazi hizo haraka iwezekanavyo kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za mikataba hiyo ili wananchi waweze kupata huduma bora iliyokusudiwa na serikali.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Hadija Nasiri alisema kuwa mikataba hiyo wataisimamia vizuri na thamani ya fedha itaonekana.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI