Na Shemsa Mussa -Matukio daima App
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa kwa Kagera imerudisha kiasi cha sh.milioni 4.3 fedha ambayo ilitakiwa kulipa wanufaika 139 wa mpango wa kunusiru kaya masikin katika kijiji cha kumtama Wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
Hayo yamesemwa leo na naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoani hapo Ezekia Sinkala wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu kwa mwezi April hadi Juni mwaka huu kwa vyombo vya habari mjini Bukoba.
Sinkala amesema,fedha hizo zilichukukiwa na wasimamizi wa zoezi la ufaulishaji wa fedha za TASAF kwa kipindi cha mwezi mei hadi Juni na julai na Agasti ikiwa ni mgao wa madirisha mawili.
Amesema,taarifa za ubadhirifu huo zilitokea katika mkutano wa hadhara uliokuwa ukihitaji kutatua kero ya Wananchi wanaonufaika nampango huo.
Amesema,baada ya kupata taarifa hizo uchunguzi ulibaini kuwa fedha husika zilizotakiwa kupelekwa ni kiasi cha sh.milioni 9.3 kwa malipo ya awamu.
"Katika ufuatuliaji ilibainika kwamba fedha husika kwa malipo ya awamu zote mbili katika kijiji cha kumtama ilikuwa sh.milioni 9.3 yaani fedha ya awamu ya kwanza ilikuwa 4.6 lakini kwa makusudi wasimamizi walitumia uelewa mdogo wa wanufaika na kujigawia fedha hizo "alisema Sinkala.
Aidha amesema,baada ya kufanyiwa mahojiano wasimamizi hao ambapo ni watumishi wawili wa Halmashauri ya ngara,mtendaji.wa kata, Mwenye kiti wa kitongoji, Mwenye kiti wa Kijiji walikiri kuwa walichukua fedha hizo na kuahidi kuludisha.
Aliongeza kuwa,wasimamizi hao walirejesha sehemu ya fedha kwa mkurugenzi wa Halmashauri hiyo na fedha hiyo ilirejeshwa kwa Wananchi ambao ni wanufaika mnamo mwaka 2021 ikiwa septemba 2020 zoezi hilo lilifanyika.
0 Comments