Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP Mufindi.
JESHI la Polisi Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa,limewataka Madereva wa magari ya Serikali Wilaya ya Mufi kujitambua kwa dhamana waliyopewa na kutokuwa chanzo cha ajali za barabarani.
Rai hiyo imetolewa na Kikosi cha Usalama barabarani Wilaya ya Mufindi na Kaimu Mkuu wa Kikosi hicho Inspekita Auson Rwehumbiza wakati akiwafunda na kuwaelimisha Madereva wa Serikali ngazi ya Wilaya.
Katika mafunzo hayo Inspekita Rwehumbiza alimwakilisha Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Wilaya ya Mufindi Afande DTO ,ASP Hassan Kimaro ,ambapo aliwataka Madereva kuheshimu taaluma yao ya Dereva na kufuata miiko ya Serikali na ajira na utumishi wa Umma.
" Tumieni kwa usahihi barabara kwa magari ya Serikali badala ya kujiona ninyi ni ninyi kwa kuendesha bila kufuata kanuni za usalama" Alisema Inspekita Rwehumbiza.
Pamoja na kuwataka Madereva kufuata kanuni na Sheria za Usalama barabarani,alisema pia wazingatie miiko yake badala ya kufanya na kuamua wanavyoona inafaa.
Madereva hao wameashwa kuacha kuendesha magari ya Serikali kwa mwendo usio rafiki kwa maisha yao ,Watumishi , Viongozi wao na watumia barabara wengine wakiwepo watembea kwa miguu.
" Madereva kumbukeni barabara ni za Umma na zinatumiwa na Jamii kubwa ya Watanzania hivi unapoendesha gari bila kuwa na tahadhari unategemea kitu gani? " Alihoji Inspekita Rwehumbiza.
Aidha Madereva hao watakiwa kuacha kuyapita magari mengine " Overtaking" bila ya kuwa na tahadhari sanjali na mwendoko kasi " Over Speed hayo haina ulazima.
" Kumbukeni magari ni mali ya Serikali na ajali inapotokea kwa uzembe Taifa linaingia hasara mara mbili au tatu kwa kupoteza uhai , mali ,ulemavu na kufanya kuwepo kwa yatima au Wategemezi ambao hawakustahili kuwepo .
Hivyo Madereva wa magari ya Serikali wametakiwa kuheshimu dhamana waliyopewa ikiwa ni pamoja na kujali maisha yao na maisha ya wengine kwa kutii Sheria bila Shuruti kwani wao ni Madereva kama walivyo Madereva wengine.
0 Comments