Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, imevuka malengo ya ukusanyaji mapato kwa mwaka wa fedha 2023/2024, ambapo imekusanya mapato kwa asilimia 116.
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la madiwani (Taarifa za kata) Jumanne Agosti 6, 2024 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. Samson Nzunda, amesema kuwa lengo lilikuwa ni kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 5.025 lakini imekusanya bilioni 5.83 ambayo ni sawa na asilimia 116.
Amesema ufanisi huo ukilinganishwa na miaka ya nyuma Kuna ongezeko la zaidi ya asilimia 10.
"Umoja wetu ndio umetufanya kuvuka lengo kwa mwaka wa fedha ulioisha ndio maana mwaka 2024/25 tumeongeza makadirio mpaka bilioni 6.6 na kutokana na vyanzo tulivyonavyo tutafikia malengo" amesema na kuongeza;
"Kutokana na vyanzo vyetu tunaweza fika bilioni 7 na angalau siku moja Mbozi iwe Halmashauri inayoongoza kwa mapato katika mkoa wa Songwe", amesema.
Katika Baraza hilo imetolewa taarifa juu ya mikakati ya ukusanyaji wa chakula kwa wanafunzi mashuleni ambapo agizo hilo limetekelezwa na shule zote zinaendelea kukusanya vyakuna na kutoa chakula kwa wanafunzi
"Serikali imekuwa ikitoa fedha kwaajili ya matengenezo ya madawati lakini bado kunaonekana kuna upungufu wa madawati hivyo, walimu walete idadi ya madawati yaliyotengenezwa", ameeleza kiongozi huyo.
0 Comments