Header Ads Widget

SHIUMA MPYA YAJA ,MATONDO AWEKWA KANDO

 

Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) kufuatia kikao cha pamoja kilichofanywa na wanachama kwa siku tatu kuanzia Tarehe 20-23 Agosti 2024 kimeamua kumweka pembeni aliyekuwa M/kiti wao wa muda Ernest Masanja Matondo na kufanya uchaguzi katika kipindi cha ndani ya miezi sita.


Akizungumza na Chombo chetu habari Katibu Mkuu  wa Shirikisho la Machinga Tanzania (SHIUMA) Ndg.Venatus Anatory amesema kikao kilifikia Uamuzi huo kutokana na Tuhuma mbalimbali zilizoibuliwa na Wanachama wa Vyama vinavyounda Shirikisho hilo ambavyo: (1) VIBINDO DAR.(2) GOWASSO (3) KAWASSO (4) UMOJA WA MACHINGA MIKOA PWANI, MOROROGORO GEITA DODOMA GEITA MBEYA NA RUKWA,

Baadhi ya Tuhuma zinazomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda Ndg.Matondo ni:(1) Kutumia Madaraka yake Vibaya (2) Kufanya Maamuzi na Ziara mbalimbali kwenye Mikoa bila Kuwashirikisha Viongozi wenzake kwa Mujibu wa Katiba.

Pia pamoja na Kujadili mambo mbalimbali Kikao hicho Kilimchagua aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Machinga Tanzania (SHIUMA) Ndg.Stephen Stanley Lusinde kuwa Mwenyekiti wa Muda kwa kipindi cha Miezi sita ambapo Shirikisho hilo litafanya Uchaguzi wa Viongozi mbalimbali kwa Mujibu wa Katiba ya Shirikisho la Machinga Tanzania (SHIUMA)


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI