Header Ads Widget

RC NJOMBE ATAKA KAMPENI YA ''TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIWA'' IFIKE KWENYE SHULE ZOTE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema shule zote mkoani hapa kutaanzishwa Klabu za masuala ya Maadili na kupinga ukatili wa kijinsia ili kuwajengea uwezo wa kutambua mabaya yanayoweza kuwakuta katika jamii.


Katika Uzinduzi wa Kampeni ya "Tuwaambie kabla hawajaharibiwa" chini ya Jeshi la Polisi mkuu wa mkoa amesema Klabu hiyo itafanya majukumu kama zilivyo Klabu za wapinga rushwa na mazingira huku akiviagiza vyombo vya usalama kuchunguza kwa kina taarifa zote zinazosikika kuhusiana na ukatili kwa watoto ili kupata ukweli.


Mtaka amesema taifa haliwezi kuwa na watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja,wanawafanyia ukatili watoto na kusababisha mmomonyoko wa maadili jambo ambalo haliwezi kufumbiwa macho katika mkoa wake.



Afande Maria Nzuki Kamishna wa Polisi Dawati la Jinsia Amesema Kampeni hiyo inalenga kuwaelimisha watoto juu ya kujilinda dhidi ya ukatili kabla hawajapatwa na madhara.


Kamishna wa Polisi Jamii Tanzania Faustine Shilogile amesema Utandawazi kwa asilimia kubwa umesababisha mmomonyoko wa maadili kwa watoto pamoja na matukio mengine ya kikatili jambo lililolifanya Jeshi la Polisi kuzindua Kampeni hiyo.



Wanafunzi Ahimidiwe Mligo Fatuma Mohamed,Irene Kulanga James Magehema wamesema wanapaswa kujiepusha na vitendo hatarishi vikiwemo vya kupokea zawadi toka kwa watu wasiowafahamu.


Kampeni ya TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIWA Chini ya Jeshi la Polisi Kitaifa imezinduliwa mkoani Njombe ikilenga kuwafikia wanafunzi wa Darasa la Kwanza kwa shule za msingi,Kidato cha Kwanza na cha Tano kwa Sekondari pamoja na Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza Vyuoni.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI