Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima App Dodoma
MWENYEKITI wa Bunge Bonanza na Bunge Marathon Festo Sanga amesema kwa kushirikiana na Benk ya NMB wanatarajia kufanya bonanza ambalo ni muendelezo ya mabonanza yote yaliopita.
Akiongea leo na waandishi wa habari Bungeni Dodoma wakati akipokea vifaa vya michezo vya bonanza hilo Mwenyekiti huyo amesema bonanza hilo litafanyika tarehe 31 Katika viwanja vya Johnmerline huku akibainisha bonanza hilo linakusudia kuleta hamasa na mahusiano na taasisi zingine.
" Kama Spika wetu wa bunge alivyoagiza Bunge tujenge mahusiano mazuri na taasisi hivyo bonanza hili linakwenda kidumisha mahusiano mema, " Amesema Mwenyekiti Sanga
Na Kuongeza " Bonanza hilo linakwenda kuunga mkono juhudi za Viongozi wa juu wa serikali za kutaka jamii kufanya mazoezi ili kuondokana na magonjwa yasiyo ya lazima ambayo yamekuwa yakiigharimu serikali kutibu wananchi.
Vile vile amesema watatumia bonanza hilo kuhamasisha watu kushiriki katika zoezi la uchaguzi mkubwa 2025 na uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa Mwaka huu, huku akibainisha kuwa bonanza hilo litakuwa na michezo tofauti tofauti ambapo wabunge na wafanyakazi wa taasisi zingine watashiriki michezo hiyo.
Kwa Upande wake Meneja NMB Kanda ya Kati Janeth Shango amelishukuru Bunge la Tanzania kulidhia kushiriki bonanza hilo ni wazi kuwa Benk ya NMB tunakubarika.
" Niwaombe tu wabunge mfanye mazoezi ya nguvu kwani Sisi kama Benk ya NMB tunakuja kushindana na hitani letu ni kushinda, " Amesema Meneja huyo.
Kauli mbiu katika bonanza hilo ni "Shiriki Uchaguzi kwa maendeleo ya nchi yetu".
0 Comments