Header Ads Widget

RAIS TLS AISHUKURU SERIKALI KUWEKA SHERIA KALI YA KUPAMBANA NA 'VISHOKA'

Na Elizabeth Zaya,Matukio Daima App 

RAIS wa Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS), Harold Sungusia, ameishukuru serikali kwa kufanya maboresho ya sheria ya mawakili sura namba 341 na kuongeza kifungu cha 41 na 42 ambavyo vimeongeza ukali wa kushughulikia ‘vishoka’ kwenye taaluma hiyo.

 Sungusia ametoa kauli hiyo jijini Dodoma katika mkutano mkuu wa TLS ambao pamoja na mambo mengine utachagua viongozi wapya wa chama hicho kesho.

Amesema kufanyia maboresho kwa sheria hiyo, kutasaidia kuendelea kusimamia na kuleta nidhamu kwa mawakili na wanataaluma hiyo kwa ujumla.

“Nishukuru serikali mwaka jana ilibadilisha sheria ya Mawakili sura namba 341 iliyorekebishwa mwaka jana kwenye kifungu ambacho kimeongeza ukali kwa vishoka na imeondoa kifungo cha miezi 12 hadi kufikia cha miaka mitatu kwa atakayejifanya ni wakili au atafanya kazi ya uwakili wakati haruhisiwi.

“Pia, faini nayo imeongezwa kutoka Sh.2000 mpaka Sh.milioni 20, kwa hiyo tunaona kwamba kuna mabadiliko makubwa na tunaamini kwamba tukiisimamia hii sheria tutaweza kupambana na wale watu wasiokuwa na maadili wanaowadanganya na kuwalaghai wananchi kwamba wao ni mawakili kumbe siyo,”anasema Sungusia.

“Kwa hiyo tunaishukuru sana serikali na kutusikiliza kurekebisha hicho kifungu cha sheria ikiwamo pia jinsi ya ambavyo tumekuwa na mashirikiano na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ofisi ya Mashtaka ya Taifa,”anasema Sungusia.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI