Header Ads Widget

NGOs TOENI ELIMU SAHIHI YA MPIGA KURA KWENYE JAMII MNAKO FANYIA SHUGHULI ZENU - DC SAME.

 


NA WILLIUM PAUL, SAME. 


MKUU wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa. 



“Niwaombe sana Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) pamoja na majuku yenu makubwa mnayotekeleza kwenye jamii ya Same lakini pia mnadhamana yingine ili nyinyi muweze kufanya kazi vizuri kwenye Mashirika yenu lazima muwe na watendaji wazuri wa Serikali" Alisema Kasilda.



Na kuongeza "lazima muwe na viongozi wenye maadili, sasa kazi yenu nyinyi kama NGOs ni kuhakikisha mnatoa elimu sahihi ya mpiga kura kwenye eneo lako unalofanyia kazi ili wananchi washiriki kikamirifu katika mazoezi yote ya uchaguzi”.



November 27-2024 nchini Tanzania kunatarajiwa kufanyika tukio kubwa la kikatiba ambalo ni Uchaguzi wa Serikali za mitaa upande wa Tanzania bara, Kampeni kwa wagombea wa vyama vyote vya siasa vitakavyoingia kwenye kinyang’anyiro hicho zitafanyika siku saba kabla ya tarehe na siku ya uchaguzi, huku zoezi la upigaji kura litaanzai saa mbili kamili asubuhi na kukamilika saa kumi kamili jioni.



Uchaguzi huu umebeba kaulimbiu isemayo “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki”. Shime wakazi wa Same mnaombwa kutumia nafasi hii kuchagua viongozi bora watakao wawakirisha vyema kweye miaka mitano mingine.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI