Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP - Dodoma
NAIBU WAZIRI wa mambo ya ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Cosato Chumi (Mb.) amefungua kongamano la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA) linalofanyika katika Chuo kikuu cha Dodoma.
Mhe.Chumi amemwakilisha Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mahmoud Thabiti katika kikao hicho la Kiswahili Afrika Mashariki.
Mhe.Chumi alisema kongamano hilo linaloongozwa na Kauli mbiu isemayo "Lugha ya Kiswahili kwa Maendeleo Barani Afrika" ikijumuisha Wataalamu ,Watafiti na Wadau wa Kiswahili wa Kiswahili kutoka Nchi za Afrika Mashariki na sehemu mbali mbali duniani.
Awali akifungua kongamano hilo Mhe.Chumi alisema Kiswahili kimekuwa miongoni mwa lugha inayotuunganisha Waafrika hususan waliopo kusini mwa jangwa la Sahara.
" Ikumbukwe kuwa Kiswahili ni lugha ambayo imeleta mchango mkubwa sana wakati wa harakati za kupigania uhuru katika katika jangwa hili la kusini mwa Afrika." Alisema Chumi.
Akizungumza nafasi ya Wizara katika kueneza lugha ya Kiswahili Ulimwenguni Mhe.Chumi ameeleza Wizara kwa kushirikiana na Wadau mbali mbali wa ndani na nje.
"Nchi ilitoa mchango mkubwa katika kukifanikisha Kiswahili kuwa lugha ya kwanza Afrika kutambuliwa na Shirika la Elimu ,Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO ).
Hata hivyo ameongeza kusema kuwa licha ya mchango huo ,Wizara ya Mambo ya Nje inaendelea kikipa kipaumbele cha pekee Kiswahili kupitia sera mpya ya mambo ya nje ,Inayofanyiwa mapitio hatua ambayo itachangia kuipa kubidhaisha lugha hiyo adhimu duniani ya Kiswahili na kuongeza matumizi ya lugha hiyo ya Kiswahili nje mipaka yetu.
" Kwa sasa Wizara yetu Ipo kwenye hatua za mwisho za mapitio ya Sera ya mambo ya nje ya Taifa letu, na kutokana na tathimini tuliyoifanya kwenye mapitio ,tumekubaliana kuongeza mawanda ya Diplomasia ya Uchumi kwa kujumuisha maeneo ambayo siyo ya jadi ( traditional) ikiwemo masuala ya kubidhaisha Kiswahili " Alisema Mhe.Chumi.
Aliongeza kusema kuwa Wizara kwa siku za usoni inatarajia kuongeza WiGo wa upatikanaji wa fursa kwa Walimu wa Kiswahili na Wakalimani sehemu mbili mbali duniani pamoja na uuzaji wa Vitabu vya Kiswahili.
Aidha upande wake ,Mratibu wa Kongamano hilo Dkt Zainabu Idd ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuolendekea kuenzi na kukuza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Alisema Tanzania inaonyesha kwa vitendo katika kukienzi na kukikuza Kiswahili duniani na kushauri kasi hii izidi kutanua kwa kasi ili lugha ya Kiswahili iweze kuzungumzwa kwa ufasaha na Mataifa yote Ulimwenguni.
0 Comments