Katika programu ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ambayo imefanyika Lindi Mjini ambayo inajulikana kwa jina la "Imarisha Uchumi na Mama Samia " (IMASA), Mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ameeleza kuwa licha ya zoezi la utoaji wa Mikopo kwa wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu kusitishwa kwa muda kwa ajili ya uboreshaji, Mkoa wa Lindi uliendelea kutenga fedha hizo ambazo hadi sasa zimefika kiasi cha Bil 3.6 .
" Niseme tu kwamba mpaka kufikia leo, Mkoa wetu unatakribani Bil 3. 6 ambazo zimetengwa kwa ajili ya kuwakopesha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu " Mhe Ndemanga.
Fedha hizo zimetengwa kutoka kila Halmashauri ambazo zinatolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu .
Mhe. Ndemanga amesema kuwa kutokana na dhamira ya serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha inaendelea kuwawezesha wananchi kiuchumi katika makundi husika imekuja na mpango wa Imarisha uchumi na Mama Samia (IMASA) ambao katika hatua ya awali imejikita katika kukusanya maoni ya walengwa kuhusu vipaumbele vya mkoa na kuwasajili.
Wajasiliamali kutoka wilaya zote wameshiriki semina hiyo na kuweza kutoa maoni na kujisajili katika mfumo ambao utawasaidia kutambulika na kupata fursa mbalimbali.
Kwa upande wake katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi. Beng'i M. Issa amesemar kuwa madhumuni ya programu hiyo katika hatua ya awali kupata takwimu za wananchi kwenye maeneo yao husika na shughuli zao katika maeneo hayo, kupata Mahitaji ya kiuchumi kwenye maeneo husika kwa kushirikiana na viongozi wa Mikoa na Wilaya, kujenga uwezo wa wananchi wote wenye uhitaji kwenye maeneo husika, kutekeleza programu ya kuwezesha wananchi kwenye Mikoa na maeneo yao.
Katika awamu hii ya kwanza itahusika katika uandaaji wa kanzi data ya walengwa/wanufaika wa programu ya IMASA.
Wakizungumza mara baada ya semina hiyo wajasilimali kutoka wilaya za Mkoa wa Lindi wameshukuru kwa programu hiyo ambayo inakwenda kuwainua kiuchumi4
0 Comments