MJUMBE WA HALMASHAURI KUU TAIFA ,MNEC Salim Abri Asas amekemea tabia ya vitendo vya rushwa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu, ili kuweka mizania sawa kwa Wagombea wakati utakapo fika.
" CCM inajicho kali kwani kuna dalili za Watu kuanza kupita pita huko bila kuzingatia taratibu na kanuni za Chama ,kawapimeni wakati ikifika na sio sasa." Alisema ASAS.
Alisema kuna viashiria ya harufu ya vitendo rushwa kwa baadhi ya Viongozi wanaotaka Uongozi katika nafasi mbali mbali.
Akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Mufindi ,alisema tabia ya kuanza kubeba mabegi ya Watia nia.
Wakati wa kampeni bado hao wanao jizungusha ujasiri huo wanapata wapata wapi naomba ujumbe uwafikie wote bila kupepesa macho hao ni wabaya ndani yake" Alisema ASAS .
Allsema kanuni za Chama lazima zifuatwe ili kuhakikisha Kiongozi bora anapatikana kwa halali na kwa mapenzi ya Wananchi na si kwa mbeleko na mabegi ya Watia nia .
Tabia ya kutaka Uongozi kwa fedha ni hatari na inachangia mgawanyiko ndani ya Chama , hali inayokifanya Chama kuwa na ugumu wa kuwanadi Viongozi kwa Wananchi.
"Wajumbe hakikisheni kuwa mnapata Viongozi wanao kubalika na wenye sifa za kweli badala ya Viongozi mnao wataka" Alisema ASAS.
"ASAS KUPIGA JEKI UJENZI WA OFISI ZA CCM KATA ZOTE WILAYA YA MUFINDI."
ASAS awali kabla ya kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Mufindi ,alitembelea Ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Upendo Mafinga Mjini na kufurahishwa na jitihada za makusudi za Ujenzi huo zinazofanywa na Wadau wa Mufindi.
Alisema amefurahishwa na Mwanachama Binti mdogo Jasmin Ng'umbi for aliyepata maono ya kutafuta fedha kwa Wadau kwa ajili ya Ujenzi wa ofisi hiyo.
Akisoma taarifa fupi ya Ujenzi wa ofisi hiyo kwa MNEC SALIM ABRI ASAS Katibu wa Siasa na Uenezi Kata ya Upendo Ndugu Octavian Alfred Mtewa alisema Kata ya Upendo ilizaliwa kutoka Kata ya Kinyanambo mwaka 2015 ,na haikuwa na ofisi yoyote kuanzia tawi hadi Kata pamoja na kuwa na Matawi mitano.
Mwezi Kata ya Upendo Mtewa alisema June 26 mwaka 2024 Wana CCM katika Kata hiyo waliitisha harambee na kumualika Ndugu Jasmin Ng'umbi kuwa mgeni rasmi ambapo walifanikiwa kukusanya kiasi cha T.sh milioni 1.7,ahadi ikiwa T.sh.3.1 milioni ,mifuko ya Simenti 68 na trip 4 za mawe.
Aliongeza kuwa katika fedha hizo Ndugu Agrey Tonga Mwenyekiti wa UVCM Mkoa alichangia 1.5 milioni na Mhe.Cosato Chumi Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini amechangia sh.500,000 .
Hivyo Katibu wa Siasa na Uenezi Kata ya Upendo Ndugu Octavian Alfred Mtewa alimwambia MNEC SALIM ABRI ASAS kuwa hadi sasa Ujenzi huo umegharimu jumla ya sh.milioni 4.1 na kwamba makadilioni hadi kukamilika ni sh.26 milioni.
Akihitimisha MNEC SALIM ABRI ASAS alimpongeza Ndugu Jasmin Ng'umbi kwa hamasa yake katika Mchango huo na kuwapongeza Wadau wengine wa Maendeleo ambao ni Wana CCM akiwepo mfanyabiashara Chesco Ng'umbi CF kwa Moyo wao wa kukisaidia Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mufindi.
MNEC ASAS alimpongeza na kumteua Jasmin Ng'umbi kuwa Mratibu wa majengo ya CCM Kata Wilaya ya Mufindi na kuahidi kumalizia Ujenzi wa ofisi hiyo ya Kata.
" Kuanzia leo nakupa kazi ya kuzunguka Wilaya ya Mufindi yote kupitia ofisi za CCM Kata na kutoa mapendekezo ya Ujenzi na nitaipiga Jeki Wilaya ya Mufindi kwa Ujenzi wa ofisi hizo .
...
0 Comments