MJUMBE wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa (NEC) Salim Abri Asas amefanya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya mchepuko ya mji wa Iringa kati ya Igumbilo -Tumain na kuagiza ujenzi wa barabara hiyo ambao umesimama kwa muda mrefu kukamilishwa kwa wakati ili kusaidia kupunguza msongamano wa magari katikati ya mji wa Iringa .
MNEC Asas alisema awali maombi ya wananchi wa mji wa Iringa na viongozi ilikuwa ni kuiomba serikali kuwezesha ujenzi wa barabara hiyo ila serikali sikivu ya chama cha mapinduzi chini ya Rais wa awamu ya sita Dkt Samia Suluhu Hassan ilisikia ombi hilo la wananchi wa Iringa na kutenga fedha zaidi ya shilingi bilioni 41 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo na tayari mkandarasi wa kujenga barabara hiyo amekwisha patikana hivyo kwa sasa CCM inatamani kuona ujenzi huo unakamilika haraka.
Kwani alisema kuwa iwapo barabara hiyo itakamilika kwa wakati itakuwa na faida kubwa kwa wananchi wa mji wa Iringa pia kwa mikoa ya nyanda za juu kusini ambao wanatumia barabara hiyo kuelekea mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini na nchini za kusini mwa Afrika ambao wanatumia barabara hiyo kupitia Dodoma ,Arusha na nchi kama za Kenya na Uganda .
" Serikali yetu ya awamu ya sita chini ya Rais wetu mpendwa Dkt Samia Suluhu Hassan tayari imetenga fedha kwa ajili ya ujezi wa barabara hii ambayo ni barabara muhimu sana kwetu wana Iringa hivyo niwaombe wale ambao wamepewa kazi ya ujenzi wa barabara hii kufanya kazi hii kwa uadilifu mkubwa na haraka zaidi ili iweze kusaidia wananchi " alisema .MNEC Asas
Hata hivyo akizungumza na wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Iringa mjini MNEC Asas alisema kuwa chama hicho kitaendelea kushinda chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani iwapo wana CCM wataungana na kuwa kitu kimoja na wenye kukitazama chama na sio kujitazama wao wenyewe kwani chama hicho ni kikubwa kuliko mtu mwana chama yeyote .
Hivyo aliwataka viongozi wa CCM waliochaguliwa na wananchi kutotembe mabega juu wakitaka wanachama kuwaheshimu wao pasipo kufanya kazi ila wanapaswa kujinyenyekeza kwa wanachama na kutekeleza majukumu yao na ilani ya uchaguzi kwa kuzingatia misingi ya chama hicho .
MNEC Asas alisema kuwa chama chochote cha siasa ni kutawala hivyo ni lazima kila kiongozi wa CCM kuhakikisha anawajibika na kutimiza malengo ya chama hicho kwa kutekeleza vyema ilani ya uchaguzi kwa kuwatumikia ipasavyo wananchi na si vinginevyo .
0 Comments