Header Ads Widget

EWURA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI MAONESHO YA 30 NANENANE JIJINI ARUSHA.

Na,Jusline Marco;Arusha


Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji imeendelea kutoa elimu kwa watanzania katika Maonesho ya 30 ya Kilimo na Sherehe za Nanenane 2024 Kanda ya Kaskazini yanayoendelea jijini Arusha ili kuboresha maisha ya mtanzania.


Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini Mhandisi Lorivii Long'idu ameyasema hayo katika ufunguzi wa maonesho hayo jijini Arusha, kuwa ushiriki wao umelenga kutoa elimu na kuwajulisha watanzania majukumu ya mamlaka hiyo ikiwemo uwekezaji wa vituo vya mafuta vya gharama nafuu.


Amesema kuwa ufanuaji biashara ya mafuta kwa kutumia miundombinu isiyo stahiki ikiwemo uuzaji wa mafuta katika chupa ni hatari kwa usalama wa mtu binafsi,mali na chombo kinachotumia mafuta hayo.


Aidha ameongeza kuwa pamoja na majukumu waliyonayo wanajukumu pia la utatuzi wa migogoro kwenye bidhaa wanazozidhibiti ikimwemo masuala ya maji na usafi wa mazingira.


Awali akifungua maonesho hayo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amewataka wananchi kujitokesha kwa wingi kwenye maonesho hayo ili kujifunza mbinu za kisasa za kilimo na ufugaji bora unaoendana na mabadiliko ya kiteknolojia sambamba na mabadiliko ya tabianchi.


Babu ameongeza kwa kuwasisitiza wananchi kuendelea kujikita katika uwekezaji wa kilimo ambacho ndiyo uti wa mgongo wa taifa ambapo asilimia 90 ya wananchi wa Kanda ya Kaskazini wanajikita katika kilimo kwa kuwa serikali ya awamu ya 6 imeweka nguvu kubwa katika kuboresha sekta ya kilimo.


Sambamba na hayo Babu ameagiza baada ya maonesho hayo kufanyike tathimini ili kupata picha halisi na kujibu baadhi ya maswali ili yaweze kutumika na kusambazwa kwa wingi katika halmashauri.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI