Header Ads Widget

DC AFUNGA MAABARA, DUKA LA DAWA VINAVYOHATARISHA AFYA

  

Duka la dawa la Mkombozi katika eneo la Mwandiga ambalo limefungwa na Mkuu wa wilaya Kigoma kwa kukiuka miongozo ya wizara ya afya

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKUU wa wilaya Kigoma Salum Kali amefunga duka la dawa na maabara zilizokuwa zinamilikiwa na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Moshi Mkazi wa Mwandiga Halmashauri ya Mji wa Kigoma kwa kile kilichoelezwa kuwa uendeshaji wake unakiuka mwongozo wa wizara ya afya na kutishia afya za wananchi wanaofika kupata huduma kwenye vituo hivyo.

 


Mkuu huyo wa wilaya amechukua hatua hiyo baada ya kufanya ziara ya ghafla kutembelea maabara na duka hilo la dawa kufuatia taarifa ya msamaria mwema ambaye aliandika barua akieleza kuendeshwa kwa huduma hizo kwa namna ambayo aliona inahatarisha Maisha ya afya ya wananchi.

 

Akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kigoma, Chiriku Chilumba na Mganga Mkuu wa halamshauri hiyo  Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo alizifanyika kazi ikiwemo kuwashirikisha viongozi hao na kufika eneo la tukio na kujiridhisha kwamba ni kweli taratibu za utoaji huduma zimekiukwa.

 


 

Akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na taratibu ambazo zimekiukwa na kufikia hatua ya vituo hivyo kufungwa Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya Kigoma,Robert Ernest  alisema kuwa moja ya mambo yaliyosababisha kufungwa kwa maabara hiyo kutoa huduma ya vipimo vya malaria kwa kutumia darubini tofauti na miongozi ya wizara ya afya kutumia kipimo kimoja kwa Zaidi ya mtu mmoja huku usafi wake ukiwa unatia shak


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kigoma, Chiriku Chilumba alisema kuwa Kabla hatua ya Mkuu wa wilaya  alifika dukani hapo na kwenye maabara kufanya ukaguzi wao na kujiridhisha kuwepo kwa ukiukwaji huo ikiwemo watoa huduma kwenye maeneo yote mawili kutokuwa na vyeti vya ithibati vya kitaaluma lakini pia maabara hiyo imekuwa ikiendesha kliniki ya wajawazito kinyume na taratibu.

 

Alipotakiwa kutoa maelezo yake na waandishi wa Habari kuhusiana nah atua hiyo ya Mkuu wa wilaya Kigoma Mmiliki huyo wa duka la dawa na maabara aliyejitambulisha kwa jina moja la Moshi alisema kuwa hakuweza kufanya maboresho mapema kutokana na changamoto zilizokuwa zikimkabili ikiwemo tatizo la fedha.

 

Mwisho.

 

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI