Header Ads Widget

CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA KUANZA KUTOA MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO

 



Na Hamida Ramadhani matukio Daima app Dodoma


KATIKA mwaka wa masomo 2025/26 chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo na Kampasi zake zote zitaanza kutoa mafunzo kwa njia ya  mtandao kwa program za cheti mastazi mpaka Digrii. 


Hayo  yamesemwa leo jijini hapa Prof Magreth Bushesha Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri kutoka chuo cha serikali ya mitaa Hombolo alipotembelea  Banda la chuo hicho katika maonesho ya kitaifa ya wakulima na wafugaji Nzuguni Dodoma


Prof Busehasa amesema Kwasasa wanatoa mafunzo hayo kwanjia ya mtandao lakini kwa ngazi ya kozi za muda mfupi mfupi. 


"Tunatoa mafunzo kwanjia ya masafa kwa kozi fupi lakini kuanzia mwaka wa masomo 2025/26 tutaanza kutoa  kozi ndefu kwa njia ya masafa kwa kozi zote cheti, diploma na digrii hivyo niwakaribishe wadau kuja  kayika banda la chuo cha Serikali za mitaa kupata mafunzo yao, vyeti vyao na digrii zao, " Amesema Prof Bushesha. 


Amesema katika kozi fupi wananzozitoa zimechangia kwa kiasi kikubwa kiboresha utendaji kazi kwenye sekta ya serikali za mitaa ni pamoja na mafunzo wanayoyatoa kwanjia ya furasa na vikwazo ambapo watendaji wa kata, madiwani na watendaji wote katika ngazi malimbali za serikali wanafundishwa namnagani wataweza  kuwaongoza wananchi kuona vikwazo vilivyopo katika maeneo yao  na kuzieuza kuwa furasa badala ya kusubiri serikali kuja kutatua changamoto hizo


" Tumefarijika kuona watendaji we tu sasa nanjinsi wanavyoziangalia changamoto na kuwa furasa au namna  ya kuweza kutatua changamoto hizo moja kwa moja kabla serikali haijatia mkono wake ni jambo zuri kwa watendaji we tu sasa", amesema Prof Bushesha .


Aidha ameeleza chuo  cha Serikali za mitaa kina kamkampsi tatu ambapo  kampasi kuu Hombolo, Dodoma mjini na kampasi ingine ipomkoani Shinyanga  huku wakiwa na mpango wakwenda sehemu zingine za Tanzania ili kuweza kuwafikia wananchi wengi. 


" Tupo katika maonesho hayo kuwaonesha wananchu shughuli malimbali zinazofanywa na chuo cha serikali za mitaa Hombolo ,Shinyanga hususuni kozi zinazotolewa, " Amesema


Aidha amewataka wananchi kufika  kupata kufahamu,kuona kozi zote kuanzia ngazi ya diploma,cheti na ngazi ya Digrii ya kwanza na digrii ya pili zinazotolewa kwani chuo hicho kimejikita hasa kwenye maeneo ya uongozi. 


" Sisi tunato mafunzo kwa viongozi wa serikali za mitaa ukiona watendaji wa kijiji, wenyeviti wa vijiji, madiwani, watendaji Kata wote wanapita katika chuo chetu cha serikali za mitaa ," Amesema. 


Na kuongeza" Lakini pia sio tu tumejikita kwenye viongozi wa mitaa hapana na viongozi wote katika ngazi malimbali na anyetaka kupata mafunzo ya uongozi anakaribishwa katika chuo cha serikali za mitaa," Amesema Prof Bushesha



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI