vijana wa bodaboda wakiwa kazini ,picha hii ya mtandaoni haihusiani na tukio la ubakaji
NA. ABDALLAH AMIRI IGUNGA
Jeshi la Polisi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora limemkamata na kumfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Igunga Hassan Idd Juma (23) kwa tuhuma ya makosa mawili, kubaka na kumpa mimba mwanafunzi wa miaka 16.
Awali mwendesha mashtaka wa serikali kutoka Ofisi ya mashitaka Wilaya ya Igunga Albanus Ndunguru akimsomea mashitaka mawili mshitakiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga Edda Kahindi, aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa alitenda makosa hayo mawili kati ya Januari 1/2024 na Januari 31/2024.
Juma mwendesha bodaboda Mkazi wa Mtaa wa Mwayunge, Kata ya Igunga katika kosa la kwanza mtuhumiwa alimbaka mwanafunzi wa miaka 16 anayesoma kidato cha nne (jina tunalo) wa Shule ya Sekondari Mwayunge.
Mwendesha mashtaka alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu 130 i na 131. Kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2022 inayozuia kutenda makosa kama hayo.
Aidha, Ndunguru aliiambia Mahakama hiyo kuwa kosa la pili linalomkabili mshitakiwa ni kwamba katika tarehe hizo Januari 1/2024 na Januari 31/2024 kwa nyakati tofauti mshitakiwa alimpa mimba mwanafunzi wa miaka 16 anayesoma Shule ya Sekondari Mwayunge iliyopo Kata ya Igunga.
Alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 60 A cha sheria ya Elimu kama ilivyofanyiwa marejeo sura 353 kifungu No. 22 cha sheria No. 4.
Baada ya kusomewa mashitaka, mshitakiwa alikana kutenda makosa hayo mawili ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agpsti 23 mwaka huu, mshitakiwa amepelekwa mahabusu.
Wakati huohuo Jeshi la Polisi Wilayani Igunga Mkoani Tabora limemfikisha katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Igunga, Juma Malale Kisingila (53) mkazi wa Mtaa wa Mwayunge Kata ya Igunga mjini akikabiliwa na tuhuma ya kufanya mapenzi na mtoto wa miaka 12 ambaye ni mwanafunzi (jina limehifadhiwa).
Mwisho.
0 Comments