Header Ads Widget

ZANZIBAR INAHITAJI MAGEUZI YA DEMOKRASIA

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa Othman Masoud Othman, amesema kwamba inawezekana Zanzibar kupiga hatua kubwa kimaendeleo na kufanikiwa kuliko ilipo sasa iwapo  wananchi wataungana katika kupingania mageuzi ya demokrasia.


Mhe. Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameyasema hayo huko katika viwanja vya ziwa maboga Tomondo wilaya ya Magharib ‘B’ Unguja alipozungunza katika mkutano wa hadhara wa chama hicho akiwa kwenye muendelezo wa mikutano kwenye majimbo mbali mbali nchini.


Amefahamisha kwamba  Zanzibar ipo kwenye dhiki kubwa ya umasikini jambo ambalo linaweza kuondoka kwa wananchi kushirikiana kwenye kuleta mabadiliko kwa kuwepo viongozi wenye uwezo uzalendo na maono  ya kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kiuchumi na Zanzibar  kuondokana na umasikini .


Amefahamisha kwamba ni lazima wananchi wa Zanzibar kuungana kwa kukiunga mkono chama hicho ili kukipatia ushindi kwenye uchaguzi ujao  kwa kuwa viongozi wake wamejipambanu katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kimaendeleo.


Amesema kwamba viongozi waliopo hawapendi kuondoka madarakati kwa kuwa kuwepo kwao ni uchumi na biashara binafsi  huku nchi ikiendelea kugubikwa na dhiki kutokana na kukosekana maono ya uongozi.


Hata hivyo, alimkosoa rais mwinyi kwa kukiuka makubaliano na kutotekeleza masuala mengi yaliyokuwemo kwenye msingi wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa kutokana na kutokuwa tayari kuleta mageuzi.


Amesema kwamba hayo yanatokea kutoka na kutokuwepo dhamira ya kweli ya kutatua matatizo ya kiasiasa Zanzibar huku viongozi wakidhani kwamba hayawahusu na hawaoni kwamba ni tatizo.


Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Ismail Jussa Ladhu, amesema kwamba ajira za vikosi vya SMZ zinazofanywa hivi zinalengo la kujinufaisha kisiasa kwa kuongeza wapiga kura bila kuzingatia mahitaji, huku nchi na wananchi wakiendelea kugubikwa na umasikini na njaa.


Amesema kwamba Rais Mwinyi amekiuka ahadi zote alizomuwekea Marehemu maalim Seif kama masharti ya msingi kwa chama hicho kuingia kwenye serikali ya kitaifa ikiwemo kuteua wakuu wa wilaya na mikoa na kuongeza mjumbe wa baraza la wawakilishi sambamba na waziri Mmoja na kurekebishwa mfumo wa uchaguzi lakini yote hakuyatekeleza.


Naye Kaimu Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Mgharib  ‘B’ Kichama Asha Ali Fakih, amesema kwamba nyumba nyingi za wakaazi wa ziwa maboga zilizowekwa  alama ya X hadi sasa hawajui khatima yao jambo ambalo limewaweka wananchi hao njia panda.


Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho Shuwena Faki Haji, amesema kwamba vijana wa Zanzibar wanakosa ajira kutokana na mfumo wa elimu uliopo kutowapa vijana elimu ya maarifa ya kuwasaidia katika kupata ajira licha ya wazazi wao kuwasomesha katika hali duni ya uzundulizaji wa fedha kutoka kwenye biashara ya uzaaji wamaandazi  na vitumbua.


Amefahamisha kwamba hali hiyo itaendelea kwa wazazi kutokuwa na kikomo cha ulezi wa vijana katika utoaji wa huduma, lakini njia pekee ni kuhakikisha  vijana wote wanapata vitambulisho ili kuipata Zanzibar mpya na Zanzibar moja kwa njia ya kura muda utakapowadia.










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI