Header Ads Widget

WANGING'OMBE NJOMBE WAPITISHA DIRA YA MAENDELEO 2050

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wakati taifa likiwa katika uchumi wa kati wa chini hivi sasa,mikakati mbalimbali imeendelea kuwekwa ili kupanda zaidi kwa kupitisha dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2050  baada ya Dira ya Taifa ya 2025 kukaribia kufika tamati hapo mwakani.


Akiwasilisha mtazamo wa dira ya maendeleo ya mwaka 2050 mtakwimu wa Halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe Burton Sinene Amesema  kumekuwa na malengo yaliyojikita katika masuala ya uboreshaji maisha ya wananchi katika uchumi,Afya,Elimu na utawala bora.

Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Claudia Kitta katika kikao maalumu cha ushauri wilaya hiyo cha kutoa maoni na kupitisha Dira ya maendeleo ya mwaka 2050 amesema maendeleo yote yaliyofanyika hadi sasa yalitokana na dira inayokoma mwaka 2025 hivyo tunalazimika kuandaa mpango mwingine.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe Agnetha Mpangile na Mbunge wa Wanging'ombe Dokta Festo Dugange Wamesema Mpango huo wa maendeleo wa 2050 utakwenda kusaidia kutekeleza miradi ya maendeleo na ni jambo kubwa na la kihistoria kupitisha dira hiyo.



Wakichangia maoni ya Dira ya maendeleo ya mwaka 2050 wakazi wa Wanging'ombe akiwemo Cosmas Makune Thobias Mkane na  Magreth Kaduma Wamesema wanataka kufanyika kwa mabadiliko ya kisera kwenye mifumo ya elimu itakayosaidia vijana wanapohitimu masomo wajue namna ya kuendesha maisha badala ya kusubiri ajira huku kwa upande wa wafanyabiashara wanapaswa kuendelezwa kielimu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI