Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Kufuatiwa kushamiri kwa vitendo vya utapeli na udanganyifu wa njia ya mtandao unaofanywa na baadhi ya matapeli Jeshi la Polisi mkoani Njombe Limewatahadharisha wananchi kuongeza umakini katika matumizi ya mitandao.
Diwani wa Kata ya Utalingolo Mhe.Erasto Mpete ambaye ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe anasema vitendo vya utapeli wa njia ya mtandao umekuwa ukiwarudisha nyuma wananchi kimaendeleo na hivyo ameliomba Jeshi la Polisi kutoa elimu juu ya matumizi ya mitandao kupitia sheria ya uhalifu mtandaoni [Cyber Crime].
Katika ufungaji wa Ligi ya Mpete Diwani Cup kata ya Utalingolo iliyompata bingwa Utalingolo FC na kujinyakulia Kombe na fedha shilingi laki tatu amesema amemualika kamanda wa Polisi ili asaidie kutoa elimu ya makosa ya mtandao kwa vijana kwa kuwa ndio wenye nafasi kubwa ya kutumia mitandao.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga akiwa Utalingolo amewataka vijana kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao kwani yanaweza kuwaingiza matatani.
Mtendaji wa Kijiji cha Utalingolo Elia Chilatu anakiri kutokea kwa matukio ya uhalifu mtandaoni huku naye akiomba elimu kutolewa hasa katika maeneo ya vijijini.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Utalingolo akiwemo Eliotel Ngilangwa na Asa Mwaipyana wanasema matapeli hao wamekuwa kikwazo kikubwa katika ukuaji wa uchumi na wamekuwa wakiwarudisha nyuma Kimaendeleo.
Matukio ya uhalifu wa mtandao yamekuwa yakitokea mara kwa mara kwa wananchi kutepeliwa fedha zao jambo ambalo sheria ya mitandao inapaswa kutekelezwa kikamilifu.
0 Comments