Na, Matukio daima App, Iringa
Zaidi ya shilingi milioni 500 kutumika katika ujenzi wa mradi wa maji safi na salama, ambao utawanufaisha, wakazi takribani 9600 kutoka kata tatu za wilaya ya Iringa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mkoani Iringa (IRUWASA), Mhandisi David Pallangyo amesema hayo wakati wa hafla fupi ya utiaji saini, ujenzi wa mradi huo wa maji safi na salama huku akitaja maeneo ambayo yatanufaika na mradi huo kuwa ni wakazi wa kata ya Kalenga, Mseke, Luhota na Kiwele.
Aidha, Mhandisi Pallangyo amesema ujenzi wa mradi huo ni utekelezaji wa maagizo ya serikali ya kutaka kuwaondoa wananchi na adha ya maji hasa wanawake ambao mara nyingi wamekuwa ndiyo wahanga wa kufuata maji, umbali mrefu.
Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiwaji saini huo Mbunge wa Kalenga Jackson Kiswaga na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya maji ya bunge, amesema ujenzi wa mradi huo ni utekelezaji wa dhamira ya dhati ya serikali ya awamu ya sita chini ya rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka kumtua mama ndoo kichwani.
Kiswaga amempongeza, Mkurugenz Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mkoani Iringa (IRUWASA), Mhandisi David Pallangyo kwa utendaji wake bora wa kazi hadi kupelekea mamlaka hiyo kuongeza maeneo ya kiutendaji ikiwemo jimboni kwake.
Akizungumzia changamoto ya malipo ya fedha za miradi kwa wakandarasi hapa nchini, mbunge huyo amesema bado serikali inaendelea kuangalia namna bora ya kuwalipa ili miradi yote ya serikali iendele kutekelezwa kwa wakati.
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Steven Muhapa ameelezea furaha yake juu ya mradi huo, pamoja na kumuahidi mbunge huyo, usimamizi mzuri wa miradi yote ambayo serikali inatoa fedha kwaaajili ya maendeleo ya wananchi.
Kwa upande wake, diwani wa kata ya Kalenga, Shakila Kiwanga amemshukuru mbunge wa jimbo la kalenga pamoja na mhandisi wa mamlaka ya maji (Iruwasa) mkoa wa Iringa kwa kusimamia zoezi hilo na kuongeza kuwa ujenzi huo unatokana na usimamizi bora wa serikali ya awamu ya sita.
Kwa upande wake mkandarasi wa mradi huo ameiomba serikali kuwezesha utoaji wa fedha za ujenzi huo kwa wakati ili kumrahisishi utendaji wake wakazi na kukamilisha ujenzi wa mradi kwa wakati.
0 Comments