Mjumbe wa Taifa wa baraza la mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali (NaCoNgo) mkoa wa Iringa Fidelis Filipatali amewataka wajumbe wa baraza hilo kufanya kazi kiwa udshirikiano ili kuwezesha ufanisi ili kuwezesha NaConGo kutambulika zaidi kwa jamii.
Akizungumza leo wakati wa mkutano wa kwanza wa NACONGO uliofanyika ukumbi wa Iringa Sun Set Hotel mwenyekiti huyo alisema kuwa kuwa lengo la serikali kuunda baraza hilo ni kutaka mashirika kufanya kazi zao pasipo kuingiliwa na serikali kwa lengo la uratibu na kuwa na kusimamia shughuli zao wenyewe.
Hivyo alisema kupitia Baraza hilo wajumbe Wanapaswa kufanya kazi kama timu Moja ili kuwezesha Baraza hilo kuwa na mafanikio makubwa na kuwa tofauti na maeneo mengine .
Alisema kuwa pamoja na NACONGO kujulikana kitaifa ila huku chini bado haijajulikana vilivyo hivyo kwa upande wa mkoa wa Iringa wamejipanga kuitambulisha vema kwa jamii ili kila mmoja afahamu majukumu ya NACONGO na kazi hiyo inahitaji ushirikiano kwa wajumbe na viongozi wote .
Filipatali alisema kuwa NACONGO mkoa wa Iringa imekusudia kuendelea kufanya kazi na serikali ili kwa pamoja kufanikisha kutoa huduma bora kwa umma.
Hata hivyo mwenyekiti huyo mpya wa NACONGO mkoa wa Iringa ambae amepokea kijiti kutoka kwa mtangulizi wake John Kiteve alisema ataendelea kufanya kazi kwa kushirikisha wajumbe na vikao na mikutano itakuwa sehemu ya utendaji wake kazi .
Katika hatua nyingine Filipatali alisoma barua ya utambulisho kutoka Taifa ambayo inamtambulisha Rasmi ngazi ya mkoa huku akiomba kwa upande wa mkoa kushusha utambulisho wa viongozi wa NACONGO ngazi za Halmashauri ili pia watambulike.
Awali mtangulizi wake kwa nafasi ya uenyekiti John Kiteve alimpongeza mwenyekiti huyo mpya kwa maono yake na jinsi alivyoanza kazi kwa vitendo na kuwa kwa upande wake toka amekuwa mwenyekiti wa NACONGO mkoa wa Iringa hajawahi kuitisha mkutano kama huo zaidi ya kukutana mitaani .
Wajumbe wa mkutano huo wakiongozwa na Lediana Mafulu Mng'ong'o waliomba ofisi ya msajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoa wa Iringa kusaidia kupatikana kwa ofisi ya NACONGO mkoa wa Iringa ndani ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa ili kuwezesha kufanya kazi kwa pamoja huku akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuyatambua mashirikana hayo.
Msajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoa wa Iringa Saida Mgeni alisema kuwa mkoa wa Iringa una mashirika yasiyo ya kiserikali zaidi ya 400 ila upatikanaji wa mashirika hayo huwa mgumu sana pale yanapohitajika kutoa taarifa zao hivyo kupitia NACONGO itakuwa rahisi zaidi kuyapata iwapo watapata ofisi ndani ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa .
Alisema kwa mwaka Jana alipata changamoto ya Baraza hilo la NACONGO kutokutana kwa zaidi ya Miaka miwili hivyo anategemea Kwa sasa haitatokea tena.
Mwenyekiti wa NACONGO na wajumbe wake
Mjumbe Jane Mwalembe
Mjumbe mstaafu wa NACONGO Mkoa wa Iringa John Kiteve akitoa neno
Mjumbe wa Baraza la NACONGO Mkoa wa Iringa Lediana Mafulu akimpongeza Msajili wa NGOs mkoa wa Iringa
Mwenyekiti wa NACONGO Mkoa wa Iringa Fidelis Filipatali katikati akiwa na wajumbe wa Baraza hilo na Msajili wa NGOs mkoa wa Iringa Saida Mgeni wa pili kushoto
Mkurugenzi wa Iringa Sunset Hotel akimpongeza mjumbe wa Taifa wa NACONGO Mkoa wa Iringa Fidelis Filipatali (kulia)

0 Comments