Header Ads Widget

VINGUNGUTI SUALA MAADILI BADO KIZUNGUMKUTI - KUMBILAMOTO ATOA USHAURI


 Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar


Wazazi na Walezi Kata ya Vingunguti wametakiwa kuwalea watoto wao katika maadili mazuri ambayo yatawejenga katika tabia njema na sio kuwa na tabia ambazo hazina sifa nzuri kwa jamii.


Ushauri huo umetolewa na Diwani wa Kata hiyo Omary Kumbilamoto ambae pia ni Meya wa jiji la Dar es Salaam wakati alipokua akiwasilisha taarifa ya ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa wananchi.


Amesema kuwa, Kata hiyo imekua ni miongoni mwa Kata ambazo zimekua na maendeleo makubwa sana ya kiuchumi katika maendeleo lakini kwenye suala la malezi wazazi bado wanasua sua jambo ambalo linapelekea kata hiyo kuwa na historia ya matukio mabaya.


"Licha ya maendeleo yote yanayoletwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh katika kata hii lakini bado suala la maadili kwa vijan limekua ni changamoto kubwa, mmong'onyoko wa maadili upo sana wazazi na walezi tujitahidi kuwalea watotl wetu vizuri"amesema Meya Kumbilamoto.


Aidha katika hatua nyengine amesema kuwa Serikali inajipanga kuleta mageuzi makubwa ya maendeleo katika Kata hiyo ikiwemo kujenga barabara za kiwango cha lami pamoja na kuongeza madarasa katika shule zilizopo katika Kata hiyo pamoja na kuongeza madawati.


"Miongoni mwa Kata ambazo zinaangaliwa kwa ukaribu na Rais wetu mpendwa Mama Samia kati ya Kata 36 zilizopo jiji la Dar es Salaam basi Vingunguti imekua ikiangaliwa kwa ukaribu zaidi katika suala zima maendeleo katika sekta ya Afya, elimu na miundombinu"amesema Meya Kumbilamoto.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI