Naibu waziri wa madini Dkt. Steven Kiruswa amefika katika jimbo la Momba mkoani Songwe kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye sekta hiyo ikiwemo uwekezaji wa madini ya Sodalite yaliyogundulika katika kijiji cha Chindi kata ya Kamsamba wilayani humo, yanayotumika kutengenezea vito vya thamani ambapo amempongeza Mbunge wa Momba Condester Sichalwe kwa ufuatiliaji wake kuona wananchi wake wananufaika.
Mbunge wa jimbo la Momba Mhe. Condester Sichalwe (Mundi) ameiomba Serikali kupitia naibu waziri huyo kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya wachimbaji wadogo kunufaika pamoja na kuinua mapato ya Serikali.








0 Comments