Header Ads Widget

TAKUKURU YAOKOA MAMILIONI IRINGA

 


Na, Matukio daima App, Iringa

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa imefanikiwa kuokoa Tsh  Milioni 49 za mkopo kutoka mfuko wa maendeleo ya Vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya kazi, Vijana ajira na wenye ulemavu.


Fedha hizi ziliombwa na mwananchi mmoja aliyedaiwa kuwa ni mkazi wa Mafinga kwa kudhaminiwa na Halmashauri ya Mji wa Mafinga ambapo, baada ya TAKUKURU kuingilia kati, ilibaini kuwa muombaji huyo hatambuliki kuwa ni mkazi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga pamoja na aina ya biashara anayodai kuifanya haifahamiki.

 

Aidha TAKUKURU ilibani kuwa muombaji alikuwa ametengenezwa ili baada ya kupokea mkopo huo atoroke na kuiachia Halmashauri ya Mji wa Mafinga deni hilo, hivyo muombaji hakupewa mkopo na fedha hizo kuokolewa.

 

Katika hatua nyingine, Takukuru mkoa wa Iringa, imefanikiwa kuokoa kiasi cha Shilingi mililioni mbili (2,000,000) kutoka kwa Maafisa wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa iringa.

 

Maafisa hao walipokea fedha hizo kutoka kwa mfanya Biashara aliyekutwa akifanya biashara bila ya kuwa na Mashine ya Kutoa Stakabadhi za kieletroniki(EFD).

 

Katika kipindi cha mwezi April hadi June 2024 takukuru mkoa wa Iringa imefuatilia utekelezaji wa miradi ya maeneleo 16 yenye thamani ya shilingi bilioni sit ana milioni mia mbili katika sekta za maji, afya, elimu, usafirishaji na ujenzi ambapo miradi mitatu iliyopo wilayani Mufindi, imekutwa na mapungufu naTakukuru imetoa ushauri kwa wasimamizi wa miradi hiyo ambayo imefanyiwa kazi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI