Header Ads Widget

SERIKALI KUTUMIA ZAIDI YA MIL. 83 KWA AJILI YA UJENZI WA JENGO LA MIONZI.

 


NA WILLIUM PAUL, SAME. 



SERIKALI kutumia kiasi cha shilingi milioni themanini na tatu laki tano (83,500,000) kwa ajili ya kujenga jengo la mionzi kwenye kituo cha Afya Hedaru Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro. 



Mradi unatekelezwa na Halmashauri ya Same kupitia nguvu kazi ya jamii (FORCE ACCOUNT) kwa kutumia fedha za Ruzuku kutoka Serikali kuu katika mwaka wa fedha 2023/24 kiasi cha shilingi milioni themanini (80,000,000) na Milioni tatu na laki tano (3,500,000) ni nguvu kazi ya jamii.


Mradi huo umeibuliwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa lengo la kuboresha huduma ya Afya na kusogeza huduma ya uchunguzi kwa njia ya Mionzi (X-RAY na ULTRASOUND) ambayo kwa sasa hupatikana kwenye Hospitali ya Wilaya hiyo pekee.



Kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuondoa adha kwa wananchi zaidi ya Elfu arobaini miasita na therasini (40,630) wa Kata ya Hedaru pamoja na wa mikoa jirani ya Tanga na Manyara waliokuwa wakilazimika kutembea umbali zaidi ya kilomita 50 kufuata huduma hiyo kwenye Hospitali ya Wilaya ya Same.


Akiwa kwenye muendelezo wa ziara zake za ukaguzi wa miradi ya maendeleo, Mkuu wa Wilaya hiyo Kasilda Mgeni amefika kwenye kituo hicho kujionea hali halisi ya utekelezaji wa mradi huo ambapo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwapatia fedha wakazi wa Same kuboresha miundomindu ya upatikanaji wa huduma bora za Afya na kwa gharama nafuu karibu na mazingira wanayoishi wananchi.



Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi moja ya wataalam wa Afya wa kituo hicho Benethson Rutahindurwa amesema ujenzi wa jengo hilo ulianza rasmi April 2 mwaka huu ambapo kwa sasa mradi upo hatua za mwisho za umaliziaji mafundi wanaendelea kuweka Vigae, PVC na Madirisha huku ukitarajiwa kukamilika July 10.


Kituo cha Afya Hedaru ni miongoni mwa vituo tisa vya Afya vya Serikali katika Halmashauri ya Wilaya ya Same vinavyotoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya upasuaji, wagonjwa wa nje, wagonjwa wa kulazwa, huduma ya kujifungua, huduma za maabara, huduma za CTC, huduma za baba, mama na mtoto, huduma za kinywa na meno, kiliniki za mkoba kwenye vijiji jirani pamoja na hudumu za mortuary.


Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI