Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi (CCM)wilaya ya Iringa Vijijini Costantino Kiwele leo kufunga maonesho ya Sabasaba kata ya Ilolompya.
Maonesho hayo ambayo yamekuwa yakifanyika Kila mwaka yamekuwa ni fursa kubwa kwa wakulima wa kata ya Ilolo Mpya na kata Jirani kutumia maonesho hayo kuonesha na kutangaza biashara zao.
Maonesho ya Sabasaba kata ya Ilolompya Kila mwaka hujumuisha mashindano ya michezo kupitia kombe la Ilolompya Cup ambalo mdhamini wake mkuu huwa ni Festo Kiswaga .
Kiswaga akiwapomgeza washindiKwa mwaka huu Kiswaga ambae ni mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa kupitia wilaya ya Iringa Vijijini na mkuu wa wilaya amedhamini kombe la mpokeaji mpira wa Miguu lililoshirikisha timu zaidi ya 15 .
Kiswaga ameiambia Matukio Daima media kuwa kwa mwaka huu ametumia kiasi Cha Tsh milioni 4 kufanikisha mashindano hayo ya soka ya Ilolompya Cup 2024 .
Kuwa zawadi zimekuwa zikiongezeka Kila mwaka na kuwa lengo ni kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kukuza michezo nchini.
Pia kuendelea kutumia mashindano hayo Kuibua Vipaji vya Vijana.
Pamoja na Kiswaga kudhamini mpira wa miguu mjumbe wa kamati ya siasa CCM mkoa wa Iringa Tumain Msowoya amedhamini mpira wa miguu kwa wanawake
0 Comments